KISHAPU WAFANYA BONANZA LA MICHEZO KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


KISHAPU WAFANYA BONANZA LA MICHEZO KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Na Marco Maduhu,KISHAPU

WILAYA ya Kishapu, imefanya Bonanza la Michezo kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Bonanza hilo limefanyika leo Novemba 23,2024 katika viwanja vya shule ya Msingi Buduhe, ambalo limefunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.

Mkude akizungumza wakati akifungua Bonanza hilo,amewataka wananchi wilayani humo,wajitokeze kwa wingi kwenye mikutano ya hadhara kusikiliza sera za wagombea,pamoja na siku ya kupiga kura novemba 27 ambayo itakuwa siku ya Jumatano ijayo.
Aidha, amewataka wananchi kwamba siku hiyo ya kupiga kura, wasifanye makosa, bali wachague wagombea makini ambao watawaletea maendeleo.

"Kupiga kura ni kuchagua maendeleo,siku ya novemba 27,jitokezeni wa wingi mkapige kura na mchague wagombea ambao watawaletea maendeleo"amesema Mkude.
Bonanza hilo la michezo litatamatika kesho novemba 24, kwa kuchezwa fainali kati ya timu ya Kishapu Secondari na Kishapu Veterani, baada ya timu hizo kuibuka na ushindi katika michezo yao

Mwaka huu,kunafanyika uchaguzi wa serikali za mitaa,wakuchagua Wenyeviti wa Vijiji,Vitongoji,Mitaa pamoja na wajumbe, ambapo Novemba 27 ndiyo siku ya kupiga kura kuwachagua viongozi hao, na sasa wanaendelea na kampeni za kunadi sera zao kwa wananchi.

TAZAMA PICHA 👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akipiga Penati kufungua Bonanza la Michezo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Joseph Mkude akisalimiana na wachezaji.


Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed akisalimia na wachezaji.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu akihamasisha wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 kwenda kupiga kura.
Viongozi wakiangalia mchezo wa mpira wa miguu kwenye bonanza hilo.
Wananchi wakiangilia mpira.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464