RC MACHA ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA,AWASIHI WANANCHI WAKIMALIZA KUPIGA KURA WARUDI NYUMBANI

RC MACHA ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA,AWASIHI WANANCHI WAKIMALIZA KUPIGA KURA WARUDI NYUMBANI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,ameshiriki kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa, huku akiwasihi wananchi mara baada ya kupiga kura, warudi majumbani mwao kusubili matokeo.
leo Novemba 27,2024 ni siku ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wa kuwachagua Wenyeviti wa Vijiji,Vitongoji,Mitaa pamoja na wajumbe, ambao watawatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitano hadi 2029.

Macha, ameshiriki upigaji kura katika kituo kilichopo viwanja vya Ikulu Kata ya Lubaga, na kutumia haki yake ya kikatiba ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, huku akiwasihi wananchi kwamba waendelee kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura, na mara baada ya kumaliza kuwachagua viongozi ambao wanawataka, warudi majumbani mwao kusubili matokeo.
“Leo ndiyo siku ya wananchi kupiga kura na kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa, na tunamshukuru Mungu hali ya hewa ni nzuri na hakuna mvua ili wananchi washiriki kikamilifu kupiga kura,”amesema Macha.

Aidha, amesema hadi sasa uchaguzi huo unaendelea vizuri kwa Amani na utulivu hakuna vurugu zozote, na kwamba kazi yao kama viongozi wa serikali, ni kuhakikisha Amani inaendelea kutawala kwenye uchaguzi huo.
Nao baadhi ya wananchi ambao wamejitokea kupiga kura akiwamo Francisca Mdingila, amepongeza utaratibu mzuri wa upigaji kura ikiwamo kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu pamoja na wazee, ambapo hawapangi foleni na kushiriki zoezi hilo kwa ufasaha.

Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami, amesema zoezi la uchaguzi katika manispaa ya Shinyanga linakwenda vizuri isipokuwa kuna dosari ndogo ndogo ambazo zimejitokeza ikiwamo baadhi ya vituo kutobandikwa orodha ya majina ya wapiga kura.
Naye Msimamizi wa uchaguzi katika Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, amesema maandalizi ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa yamefanyika vizuri ambapo kuna vituo 285.

Amezungumzia pia suala la baadhi ya vituo kutobandikwa majina ya wapiga kura, ni kwamba kwenye vituo vya wazi ambavyo vipo 149 majina hayo yajabandikwa kutokana na kuhofia mvua, na kwamba daftari lenye orodha ya majina lipo kwa wasimamizi wa uchaguzi hapo hapo kituoni, ambapo kila mtu atahakikiwa jina lake na kushiriki kupiga kura.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiondoka na Bodaboda mara baada ya kumaliza kupiga kura.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamdun akipiga foleni kupiga kura.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464