CHADEMA:KUONDOLEWA MAJINA YA WAGOMBEA WAO NI KUWANYIMA WANANCHI HAKI YAO YA KIKATIBA KUWACHAGUA VIONGOZI WANAOWATAKA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

CHADEMA:KUONDOLEWA MAJINA YA WAGOMBEA WAO NI KUWANYIMA WANANCHI HAKI YAO YA KIKATIBA KUWACHAGUA VIONGOZI WANAOWATAKA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Serengeti,kimesema kuondolewa majina ya wagombea wao kutogombea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu,ni kuwanyima wananchi haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi ambao wanawataka kuwaongoza.
Hayo yamebainisha leo Novemba 27,2024 na Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami, wakati akizungumza na waandishi wa habari,kufuatia wagombea wao kuenguliwa kutogomba kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa akidai kinyume na kanuni ya uchaguzi.

Amesema wamesikitishwa na uonevu ambao umeonyesha hadharani na wasimamizi wa uchaguzi, kwa kuondoa majina ya wagombea wao, ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa, jambo ambalo ni kuwakosea wananchi na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuwachagua viongozi ambao wanawataka na kuishia kuchaguliwa.
“Sisi Chadema katika uchaguzi wetu ndani ya Chama, tuliweka wagombea ambao wanakubalika na wananchi, sasa imekuja hofu na kuamua kuwaondoa wagombea wetu kinyume na kanuni ya uchaguzi, mfano eti mgombea anawekewa pingamizi kwanini ana wake wengi, na kuna mapingamizi mengi tu ambayo hayapo kwenye kanuni,”amesema Mnyawami.

Aidha,amesema sasa hivi wapo kwenye mchakato wa kukata Rufaa kwa wagombea wao, na zitawasilishwa kesho,na kutoa tahadhari kwa wasimamizi wa uchaguzi na Waziri wa TAMISEM, kwamba watende haki na kurudisha majina ya wagombea wao, ili wapambane majukwaani kunadi sera na kushinda kihalali kwa kuchaguliwa na wananchi.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Sebastian Polepole,amesema amesikitishwa na wagombea wao kuondolewa kutoshiriki kwenye uchaguzi huo kwa uonevu mkubwa, na wakati kabla ya kurudisha fomu zao walihakikisha zipo sawa.

Nao baadhi ya wagombea ambao majina yao yameondolewa akiwamo Mkasha John Emmanuel,amesema yeye ameondolewa jina lake akidaiwa hakutaja mtaa ambao anagombea,ambao ni kiwandani na kueleza kwenye fomu kwa nyuma inajieleza mtaa ambao anagombea, huku akieleza sababu nyingine ni kwamba alija umri tofauti na aliojaza kwenye daftari la mpiga kura.
Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, amesema hakuna Mgombea wa upinzani ambaye ameondolewa kimakosa bali wamejiundoa wenyewe kutokana na kutokidhi vigezo.

Amesema baadhi ya wagombea kwenye fomu walizojaza walikosea, na kwamba Mgombea ni wajinsia ya kiume lakini amejaza kwenye jinsia ya kike, huku wengine wakiwa hawajajiandikisha kwenye daftari la makazi la mpiga kura, pamoja na kujidhamini wenyewe badala ya kudhaminiwa na Chama.

Aidha, amesema kwa Mgombea ambaye hajaridhika na uteuzi wa majina, anayohaki ya kukata Rufaa na kupeleka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga.

Aidha,uteuzi wa majina ya wagombea ulifanyika Novemba 8, na mwisho wa kupeleka Rufaa ni Novemba 13,na uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika Novemba 27 mwaka huu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami,akizungumzia sakata la wagombea wa Chadema kuenguliwa majina yao kutogombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Katibu wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Sebastian Polepole,akizungumzia sakata la wagombea wa Chadema kuenguliwa majina yao kutoshiriki kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Katibu wa BAWACHA Agata Mamuya akizumzia Sakata la wagombea wa Chadema kuenguliwa majina yao kutoshiriki kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Katibu wa BAVICHA Joseph Shabani akizungumzia sakata la wagombea wa Chadema kuenguliwa majina yao kutoshiriki kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mkasha John Emmanuel akielezea namna alivyoondolewa jina lake kutogombea nafasi ya uenyekiti wa Mtaa wa viwandani Manispaa ya Shinyanga na kukiukwa kanuni za uchaguzi.
Wagombea wa Chadema wakiendelea kueleza namna walivyo ondolewa majina yao.
Wagombea wakionyesha fomu za kukata Rufaa kuondolewa majina yao kutoshiriki kugombea nafasi za uongozi uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464