KATAMBI ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

KATAMBI ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu,ameshiriki kupiga kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Amepiga kura leo Novemba 27,2024 katika Kituo cha Buyuni kilichopo Kitongoji cha Mlimani Kata ya Oldshinyanga, kwa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa pamoja na wajumbe.

Amesema ameshiriki kupiga kura ili kichagua viongozi hao wa serikali za mitaa, sababu mfumo wa serikali una anzia ngazi ya chini,hivyo upatikanaji wa viongozi makini ngazi ya vijiji,vitongoji na mitaa, ndiyo msingi imara wa utawala.
"Zoezi hili la uchaguzi linakwenda vizuri na wananchi wamejitokeza kupiga kura tena kwa amani na utulivu, na wasimamizi wa uchaguzi wanatoa maelekezo mazuri namna ya kupiga kura," amesema Katambi.

Aidha, amewasihi wananchi wachague viongozi makini, wanaoaminika, waadilifu,weledi na wenye kupigania matatizo yao.
Leo ni uchaguzi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania, ambapo wananchi wanachagua Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa, Kitongoji pamoja na wajumbe ambao watawaongoza wananchi kwa kipindi cha miaka Mitano hadi 2029.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu,akielekea kupiga kura.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu,akipanga foleni kupiga kura.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu akihakiki jina kabla ya kupiga kura.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu, akipiga kura.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464