MONGELLA AHITIMISHA KAMPENI ZA CCM KWA KISHINDO MKOANI SHINYANGA
Mitaa Minne, Vijiji 2,176,Vitongoji 307 wagombea wa CCM wamepita bila ya kupingwa,ambapo watapigiwa kura za ndiyo au hapana
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara John Mongella, amehitimisha kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM mkoani Shinyanga, ambao watapeperusha bendera ya Chama hicho kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utafanyika kesho Novemba 27 kwa wananchi kupiga kura ya kuchagua Wenyeviti wa Vijiji Mitaa, Vitongoji,pamoja na wajumbe.
Mongella amehitimisha kampeni hizo leo Novemba 26 katika Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga, na kuwanadi wagombea wa CCM kwa wananchi, kwamba kesho wakawapigie kura ili wapate kushinda na kuwaletea maendeleo.
“Kuwachagua Wagombea wa CCM ni kuchagua Maendeleo,Amani na Umoja, na Maendeleo ya Taifa letu yana anzia kwa viongozi wa serikali za mitaa,”amesema Mongella.
Aidha, amesema katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa, tayari Wagombea wa CCM katika Mitaa 90, Minne amepita bila ya kupingwa, na Kati ya Vitongoji 2,703 , Vitongoji 2,176 wamepita bila ya kupingwa, huku Vijiji 506,vijiji 307 wamepita bila ya kupingwa, na kuwasihi wananchi wajitokeze pia kuwapigia kura za ndiyo ili wapate kushinda kwa kupigiwa kura.
Nao baadhi ya viongozi mbalimbali wa Chama hicho wakiwamo Madiwani na Wabunge, wamewaomba wananchi wa Shinyanga, kwamba wakawachague wogombea wote wa CCM ili kuwepo na muunganiko wa uongozi na kuwaletea maendeleo.
TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara John Mongella akihitimisha kampeni za CCM Mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwa nadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwa nadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Mkombe akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwa nadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Diwani wa Kitangili Mariam Nyangaka akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.