WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE KOM SEKONDARI WATAKIWA KUEPUKA MAKUNDI HATARISHI ILI KUTIMIZA NDOTO ZAO


Wahitimu wa kidato cha nne shule ya Kom sekondari wakiburudika 


 Suzy Butondo, Shinyangapress Blog


Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hango amewataka wanafunzi wote 131 waliohitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kom iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga kuepuka makundi hatarishi ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao na kushindwa kufikia malengo yao.

Hango ameyasema leo wakati akiwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 16 ya kuhitimu kidato cha nne, ambapo amewataka wahitimu wote wanapokuwa nyumbani waepuke kujiingiza kwenye makundi hatarishi yasiyo na maadili mema katika jamii.

"Sasa mnamaliza masomo ya kidato cha nne mnaelekea nyumbani kama mlivyosema mnaenda kupumzika kidogo na kweli nendeni mkapumzike, lakini msijiingize kwenye vikundi ambavyo havina maadili mema katika jamii na hapa katika risala yenu nimesikia kuwa mmejifunza kulima mbogamboga hizo tumeziona, hivyo nendeni mkaanzishe mashamba ya mboga mboga msifuate makundi mabaya mkashindwa kutimiza ndoto zenu",amesema Hongo.

"Katika shule hii mmefundishwa nidhamu, hivyo mkaendelee na nidhamu mliyofundishwa na walimu wenu ambayo imewasaidia mpaka kufikia leo mmehitimu kidato cha nne na mmeahidi kuwa lazima mfaulu wote na mpate daraja la kwanza,  hivyo nawapongeza sana kwa kujiamini kwenu naamini hata Mungu atawasaidia",ameongeza.


Pia amewapongeza walimu kwa kuanzisha ujasiriamali wa kilimo cha mboga mboga,  hivyo amewaomba wanafunzi wajiunge wawili wawili wawe na sehemu yao ili kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa na ujuzi wa kulima mbogamboga hizo hata anapohitimu asihangaike jinsi ya kujiajiri na kujiongezea uchumi wake.

Akizungumzia changamoto zilizopo katika shule hiyo ambazo ni gharama za uendeshaji, amewaomba wazazi wote wahakikishe wanalipa ada kwa wakati kwa sababu shule inajiendesha yenyewe ni ya binafsi siyo ya serikali, hivyo ni jukumu lao wazazi kulipa kwa wakati wasisubiri mtoto arudishwe nyumbani.

"Pia ni vizuri  wazazi wakalipia bima ya afya watoto wao ili waweze kutibiwa kwa wakati wakiwa shuleni hapo, pia niwaombe muwe mnaleta taarifa kamili za wanafunzi wakati wa kusajiliwa,amesema

"Imebainika ufaulu wenu wanafunzi ni asilimia 85.4 wote mmekuwa mkienda kidato cha tano na cha sita kwa miaka sita yote, hivyo niwaombe mdumishe nidhamu, elimu mliyoipata ikasaidie kutatua changamoto za kimaisha, lakini pia msisite kujiendeleza na nyinyi katika kidato cha tano na cha sita mpaka chuo kikuu degree ya pili degree ya tatu someni tu jinsi mtakavyofanikiwa kwa sababu elimu haina mwisho,"amesema.


Mwalimu mkuu wa shule ya Kom sekondari Grace Mtabilwa amesema shule ya sekondari ilisajiliwa Januari 2006 ikiwa na wanafunzi 89 wavulana 55 wakiwa na wasichana 34 na wafanyakazi 10 walimu 6 na wasio walimu 4 kwa sasa ina wanafunzi 505 wasichana 223 na wavulana 282 walimu 40 na wasio walimu ni 20 shule ni ya kutwa na bweni na ni mchanganyiko wasichana na wavulana, shule ipo katika katika kata ya Ndembezi eneo la Butengwa manispaa ya Shinyanga.

"Dira ya shule ni kutoa elimu bora kwa vijana wote bila kujali itikadi zao za kidini kisiasa kabila na rangi mahali hapa ni sehemu huru na muafaka kwa kila mwanafunzi mwenye kiu na elimu adhima ya shule ni kuandaa mazingira mazuri ya kujifunzia ,yanayomwezesha mwanafunzi kujifunza vizuri na hatimaye kukabiliana na changamoto za baadae, "na kauli mbiu yetu ni elimu bora kwa wote"

"Katika taaluma shule yetu imefanikiwa kupata matokeo mazuri katika mitihani mbalimbali ya ndani na ya nje, tunayoifanya kwa kushirikiana na shule zingine  na matokeo yote katika matokeo ya Taifa kidato cha pili na cha nne kwa miaka sita mfululizo   yamekuwa mazuri na ya kuridhisha, jumla ya wanafunzi 2331 wamehitimu kidato cha nne kuanzia 2009 hadi  2023 kati yao  1990 sawa na asilimia 85.4 ya wahitimu wote walichaguliwa kujiunga na kidato cha tano na wengine kujiunga katika vyuo mbalimbali, matokeo haya mazuri ni juhudi za wazazi, walimu na viongozi wa shule.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Piter Kuburu amewashukuru sana wazazi kwa kuendelea kuiamini shule ya Kom sekondari na kusisitiza wazazi watoe ushirikiano kwa walimu pale wanapohitajika shuleni wafike kwa wakati kwa ajili ya maendeleo ya mtoto.

Mkurugenzi wa shule ya Kom sekondari Jackton Koyi amewataka wanafunzi wajiheshimu wawaheshimu wazazi wao wavae mavazi ya kinidhamu, watembee kinidhamu na wale kinidhamu,na wakawe watulivu wakajiheshimu na wakaheshimu muda wao na  wawasaidie wazazi.

"Vijana wangu leo mnamaliza kidato cha nne hivyo naamini huko muendako mtakuwa wawakilishi wazuri sana wa shule ya Kom, mlianza wachache na mnamaliza wengi, kama mlivyoimba kwamba maisha ya shule si simple mmekutana na changamoto nyingi, na sasa mmesema mmeweka pozi na naamini mlivyosema mtaendelea wote, na mmeahidi mtapata daraja la kwanza wote na mmeahidi mbele ya wazazi wenu hapa,"amesema Koyi.

"Hivyo na mimi ninaimani mtaendelea kwa sababu mmesema nyinyi wenyewe mtafaulu kwa asilimia 100, walimu wamewalea wamewaongoza vyema, niwaombe wazazi muwasimamie vizuri huko nyumbani ili wote waendelee na masomo ya juu, hapa wamejifunza kulima kisasa, kama kuna kanafasi kadogo ka kulima wapeni walime ili msiendelee kununua mbogamboga, wanaweza kulima,pia washirikisheni kufanya na kazi zingine,"amesema Koyi.

"Pia niwashukuru wazazi kwa kuiamini shule na kutuamini sisi kuwa sehemu ya malezi ya watoto hawa, niwaombe muendelee kutuamini, kwani hapa ni mahali salama kwa ajili ya malezi, na niwapongeze sana walezi wao wakuu walimu kwa kuwasimamia hawa vijana na leo wana nyuso za furaha, wamefanya kazi kubwa, na kwa namna ya pekee niishukuru bodi ya shule kwa usimamizi mzuri,"ameongeza.

Aidha amesema baadhi ya wazazi wamekuwa na changamoto ya kutolipa ada kwa wakati mwingine hali ambayo hulazimisha kuwarudisha watoto nyumbani, lakini walitoa fursa ya kufanya maelewano kwamba kama mzazi hawajafanikiwa fedha wakati wa kufungua shule mtoto, mzazi anatakiwa kwenda shuleni kwa ajili ya makubaliano ya kwamba atalipa lini.

"Lakini cha kushangaza wazazi wengine wanawatuma watoto waje watuambie tuwapigie simu sisi, na huku kama kuna mkwamo tunawaomba wazazi wenyewe waje ili tusiwaumize watoto kwa kuwarudisha nyumbani, hivyo niwaombe wazazi wenye watoto wanaobaki hapa tuzingatie hili, pia niwaombe wazazi mnaolipa mapema ada msiwacheleweshe kuja shule bila sababu ya msingi, hapa hatuna kazi za kufanya ni kusoma tu", amesema Koyi
Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Samson Hango akizungumza kwenye mahafali ya 16 katika shule ya Kom Sekondari 

Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari akizungumza kwenye mahafali ya 16 ya kidato cha nne 

Mwenyemiti wa bodi ya shule ya Kom Sekondari Peter Kuburu akizungumza kwenye mahafali hayo



Mwalimu mkuu wa shule ya Kom sekondari Grace Mtabilwa akisoma taarifa ya shule hiyo

Meneja wa shule ya Kom Sekondari Magreth Koyi akifurahia jambo, huku wanafunzi wakimlisha keki mgeni rasmi

Wahitimu wakiingia ukumbini kwa burudani 

Wahitimu wakiingia ukumbini kwa burudani 

Wahitimu wakiburudika kwenye mahafali yao


Wahitimu wakiburudika kwenye mahafali yao

Wahitimu wakiburudika kwenye mahafali yao

Wahitimu wakiburudika kwenye mahafali yao

wahitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Wanafunzi wa shule ya Msingi Kom wakiwa kwenye mahafali hiyo wakiimba wimbo wa Taifa

Wahitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Wahitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Wahitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Wahitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari ya wasichana Butengwa wakiwa kwenye mahafali hiyo


Wazazi wa watoto waliohitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Wazazi na wadogo zao wahitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Wazazi na wadogo zao wahitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Watoto na wazazi wakiwa kwenye mahafali

Mgeni rasm akiendelea kukagua na kupata maelezo kwa wanafunzi ambao wamejifunza mambo mbalimbali wakiwa shuleni hapo

Mgeni rasmi wa mahafali hiyo akipokea keki kutoka kwa wahitimu 

Viongozi wa shule hiyo wakipokea keki

Mkurugenzi wa shule ya Kom sekondari akiwa na meneja wa shule hiyo Magreth Koyi wakipokea keki

Wahitimu wakisoma risala kwenye mahafali yao

Watoto wa shule ya msingi Kom wakitoa burudani kwenye mahafali ya 16 ya kidato cha nne

Michezo ikiendelea katika mahafali hiyo 

Mgeni rasm akipata maelezo kwa wanafunzi, baada ya kuonyeshwa mboga mboga, nyanya na Tango zinazolimwa shuleni hapo kwa ajili ya matumizi ya shule 

Wanafunzi wakimsubiri mgeni rasim ili wamweleze jinsi vifaa hivyo walivyotengeneza vinafanya kazi gani

Mgeni rasmi akiendelea kupata maelezo kwa wanafunzi kuhusiana na vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na wanafunzi wa shule hiyo


Mgeni rasmi akipata maelezo kwa wanafunzi, baada ya kuonyeshwa mboga mboga, nyanya na Tango zinazolimwa shuleni hapo kwa ajili ya matumizi ya shule 

Mgeni rasmi akiwa na viongozi wa Kom Sekondari wakisubiri kulishwa keki

Mmoja wa wanafunzi akipokea cheti katika mahafali hiyo 

Walimu wa shule ya Kom wakisakata Rumba kwenye mahafali hiyo

Walimu wa shule hiyo wakiwa na keki yao baada ya kupokea kutoka kwa wahitimu

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464