Kupitia uchaguzi huu viongozi wa chama hicho wametakiwa
kusimamaia haki,
sheria na wajibu kwa mwalimu ili kuleta chachu kwa walimu ikiwa nipamoja na
kuhakikisha
walimu wanatekeleza
wajibu wao kwa mwajili bila kujali maslahi yao binafsi
Msimamizi mkuu wa uchaguzi kitaifa Samson Meng'anyi
amesema viongozi
wanatakiwa kuwa
mstari wa mbele katika utekelezaji wa majuku yao kisheria kwa kufuata miongozo iliyowekwa na serkali na kuishukuru serkali kwa kuiweka mifumo rafiki kwa wafanyakazi hususani kuwa na uhuru wa kuanzisha na kujiunga na chama chochote.
Akizungumza mara baada
ya zoezi la uchaguzi mkuu wa viongozi Mwenyekiti wa (CHAKUHAWATA) Manispaa ya
Shinyanga mwalimu Jonas Kapezi amesema kwa kushirikiana na viongozi waliochaguliwa katika
ngazi
mbalimbali ikiwemo
uwakailishi wa watu wenye ulemavu katika manispaa hiyo watasimamia vema
haki
za walimu kwa mujibu
wa sheria na kanuni.
Sheria ya ajira na
mahusiaono kazini sheria namba 6 ya mwaka 2004 inatoa haki ya kuunda vyama vya
wafanyakazi pia inatoa
uhuru kwa mtumishi kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi.