Lukas Yombo Katemani akiwa nyumbani kwake mtaa wa mkwajuni kata ya Somangila manispaa ya Kigamboni
Suzy Butondo, Shinyangapress blog
Lukas Yombo Katemani Mkazi wa mtaa wa Mkwajuni kata ya Somangila Manispaa ya Kigamboni Mkoa wa Dar es salaam ambaye ni mfanyabiashara amejitolea kumsomesha masomo ya ujasiliamali binti Annastazia Sayi aliyerudishwa na mme wake kwa madai hazai, na wazazi wake kudaiwa mahali iliyotolewa.
Katemani ambaye ni mkazi wa manispaa ya Kigamboni akizungumza na mwandishi wa shinyangapress blog,kwa njia ya simu ya mkononi amesema baada ya kuona malalamiko ya Petro Sayi ya kwamba mtoto wake aliolewa na kukaa miaka minne kwa mme na kutofanikiwa kuzaa, na mama mkwe kuamru arudishwe nyumbani kwao binti, na kudaiwa mahari imemsikitisha sana na kuamua kumsaidia binti huyo kwa kumsomesha masomo ya ujasiliamali.
"Niliona habari hii kwenye blog ya shinyagapress nikasoma nikasikitika sana kwani nikaona huu ni unyanyasaji ambao unamfanya mtoto wa kike akose amani na kuwa na mawazo, pia kudaiwa mahari unawafanya wazazi wakose amani kwa kudaiwa mahali ya ng"ombe saba ambao waliwapokea kwa miaka minne iliyopita,inawezekana wameshatumia, kwa sababu mahari inatolewa kama zawadi ya mzazi kwa ajili ya malezi ya kumlea mpaka kufikia umri wa kuolewa"amesema Katemani.
""Labda niseme tu kwamba zawadi ikishatolewa hairudishwi, niombe tu jamii ipewe elimu kuwa mahari hairudishwi inapotolewa kwa wazazi "ameongeza.
Aidha baba mzazi wa Annastazia Sayi, Petro Sayi amemshukuru Katemani kwa kujitoa kumsomesha binti yake kwa sababu alikuwa akiishi nae nyumbani bila kufanya shughuli zake za kujiingizia kipato hii itasaidia kumpunguzia mawazo binti yake, pale atakapomaliza masomo yake atajiingizia kipato chake.
"Namshukuru sana ndugu yangu huyu kwa kunionea huruma na kunishika mkono kwa ajili ya kumsomesha binti yangu masomo ya ujasiliamali, hii itamsaidia binti yangu kumuondolea mawazo, kwani kuna wakati anakaa na kuanza kufikilia, na ananifikilia na mimi baba yake jinsi ninavyohangaika kutafuta haki itendeke lakini inafika mahala nagonga mwamba huku nikitumia gharama kubwa kwenda mahakamani na mahakama kunihukumu nitoe mahali hizo niiombe serikali inisaidie na wadau mbalimbali nateseka sana "amesema Sayi.