Katibu tawala Wilaya Kishapu Mkoani Shinyanga Bi.Fatma Mohamed akizungumza Novemba 24,2024 kwenye kilele cha bonanza la michezo kuhamasisha ushiriki kwenye uchaguzi serikali za mitaa lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe Wilayani humo.
Mchezaji wa Kishapu Veteran akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza katika kilele cha bonanza la michezo kuhamasisha ushiriki uchaguzi serikali za mitaa. Picha na Sumai Salum
Wachezaji wa Kishapu sekondari wakipokea zawadi ya mshindi wa pili katika kilele cha bonanza la michezo kuhamasisha ushiriki uchaguzi serikali za mitaa.
Na Sumai Salum - Kishapu
Bonanza la michezo la kuhamasisha ushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa lililoanza Novemba 23, 2024, na kuhitimishwa Novemba 24, 2024, limefanikiwa kuvutia umati mkubwa wa wananchi wilayani Kishapu.
Katika bonanza hili, timu ya Kishapu Veteran imeonyesha umahiri wake na kutwaa ushindi wa kwanza kwa kuifunga Kishapu Sekondari magoli 4-1.
Akizungumza kwenye hafla ya kufunga bonanza hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Bi. Fatma Mohamed, aliwashukuru wananchi kwa ushiriki wao mzuri na aliwasisitiza kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Amesema, "Ndugu zangu wananchi, mmelifanya bonanza hili kung'ara, hivyo wote mliofikisha umri wa miaka 18 na kuendelea na waliojiandikisha, tuhakikishe kuwa tarehe 27, 2024 tunaenda kwenye vituo vyetu elekezi kupiga kura na kuchagua viongozi watakaotuletea maendeleo katika taifa letu."
Bi. Fatma pia ametoa pongezi kwa timu zote zilizoshiriki katika michuano hiyo, akitaja Kishapu Veteran kama mshindi wa kwanza, Kishapu Sekondari kama mshindi wa pili, Igaga Combine kama mshindi wa tatu, na Bodaboda FC kama mshindi wa nne.
Amewatambua kwa kujitolea kwao na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata nafasi ya kutimiza haki yake ya kikatiba.
Zawadi kwa washindi zilikuwa ni pamoja na kikombe cha ubingwa, fedha za zawadi, mipira, na vyeti vya ushiriki.
Kishapu Veteran ameshinda zawadi ya Tsh. 150,000, mpira na cheti cha ushiriki, huku Kishapu Sekondari wakiibuka na Tsh. 100,000, mpira na cheti cha ushiriki. Washindi wa tatu na wa nne wamekabidhiwa mipira na vyeti.
Bonanza hili lilizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Mkude, ambaye aliwashukuru wananchi kwa kuonyesha mshikamano na kujitolea kwa dhati katika kuhamasisha ushiriki wa uchaguzi.
Bonanza limehitimishwa kwa furaha na hamasa kubwa ya wananchi kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024
Watumbuizaji almaarufu "Mdudu" wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakitumbuiza kwenye bonanza la michezo kushiriki uchaguzi serikali za mitaa lililohitimishwa Novemba 24,2024 katika viwanja vya mpira shule ya msingi Buduhe Wilayani humo.
Mwenyekiti wa michezo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Sospeter Kundwa akizungumza kwenye viwanja vya mpira shule ya msingi Buduhe kwenye tamati ya bonanza la michezo kuhamasisha ushiriki uchaguzi serikali za mitaa lililozinduliwa Novemba23,2024 na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Joseph Mkude na kuhitimishwa Novemba 24,2024 na Katibu tawala Bi.Fatma Mohamed.
Afisa wa Takukuru Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga George Kasyanjo akitoa elimu ya kuzuia na kupambana kwa wananchi walioudhuria bonanza hilo Novemba 24,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa jumatano Novemba 27, 2024
Picha ya pamoja ya meza kuu na timu ya Kishapu sekondari kabla ya mchezo wao Novemba 24,2024
Picha ya pamoja ya meza kuu na timu ya Kishapu Veteran kabla ya mchezo wao Novemba 24,2024
Afisa utamaduni Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Queen Mwajilala akifurahia kuona mchuano kati ya Kishapu Veteran na Kishapu sekondari Novemba 24,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe kwenye tamati la bonanza la michezo kuhamasisha ushiriki uchaguzi serikali za mitaa.
Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Wilaya Kishapu Mkoani Shinyanga bi.Atuganile Stephen akifuatilia bonanza la michezo
Afisa tawala Wilayani ya kishapu Mkoani Shinyanga Fadhiri Mvanga akizungumza Novemba 24,2024 kwenye kilele cha bonanza la michezo kuhamasisha ushiriki uchaguzi serikali za mitaa lililofanyika katika viwanja vya mpira shule ya msingi Buduhe.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464