KLABU ZA HABARI ZIMEKUZA SEKTA YA ELIMU NA TEKNOLOJIA NCHINI
Picha ni wajumbe wa Bodi ya UTPC wakiwa na makatibu wa klabu za habari nchini.
Na Kareny Masasy,
Singida.
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Tecknolojia Adolf Mkenda amesema mshikamano na waandishi wa habari hapa nchini umeweza kunyanyua Sekta ya Elimu na kukuza Tecknolojia.
Mkenda amesema hayo leo tarehe1,Novemba,2024 alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa wanachama wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC ) uliofanyika mkoani Singida.
Mkenda amesema jamii lianza kusema hivi Sasa elimu imeshuka kwa kuondoa kutangaza shule bora,mwanafunzi bora lakini jambo hilo kupitia vyombo vya habari wananchi walielezwa.
"Wizara yetu tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano kwani nimekuwa nikitumia vyombo vya habari hata pale kunapohitaji ufafanuzi wa jambo fulani la kielimu hasa linalokuwa na mabadiliko kwenye jamii"alisema Mkenda.
Mkenda amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu alisema katika Sekta ya Elimu ataleta mabadiliko makubwa kuhakikisha elimu inaboreshwa na kuwa bora kwa kuanza na mabadiliko ya mitaala.
"Mageuzi yote tumeyafanya kwa shule za msingi katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ila elimu ya msingi itakuwa ni lazima katika mtaala mpya hivyo mtoto lazima aanze na amalize"amesema Mkenda.
Mkenda alisema mwanafunzi wa darasa la awali,kwanza na tatu wameanza na mtaala mpya na aliye darasa la pili akiingia darasa tatu ataanza na mtaala mpya na kuendelea mpaka darasa la sita na lazima amalize elimu ya Sekondari najua Serikali inapotekeleza itakuwepo changamoto hakuna kukata tamaa.
Mkenda alisema kutakuwa na mkondo wa amali na ufundi ambapo wakimaliza elimu ya Sekondari watasoma masomo matano na watafundishwa ujasiriamali na mwisho watapata Cheri ambacho atakutumia hata kuomba kazi.
Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya amesema Sekta ya Elimu wamekuwa wakishirikiana nayo kuanzia ngazi ya awali hivyo wataendelea kufuatilia kuhakikisha waandishi wa habari wanapata wasaa kukualika Tena ili waulize maswali.
Wajumbe wa klabu ya habari mkoa wa Shinyanga na Rukwa wakiwa na viongozi wa juu wa UTPC