MADIWANI KISHAPU WAIOMBA BODI YA PAMBA KUWAONGEZEA MBEGU ZA PAMBA ILI KUKIDHI MAHITAJI YAO


Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwakwenye kikao cha baraza


Suzy Butondo,Shinyanga press blog

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga wameiomba bodi ya pamba kuwaongezea mbegu za pamba, kwani walizogawiwa hazikidhi mahitaji yao kulingana na mashamba yao waliyoandaa kulima.

Hayo wameyasema kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, ambapo wamesema mbegu zilizogawiwa ni kidogo, hivyo kuitaka bodi hiyo iwaongezee ili kutimiza mahitaji yao.

Diwani wa kata ya Bubiki James Kasomi na diwani wa kata ya Mwamashele Lukas Nkende wamesema katika maeneo yao wananchi bado hawajapata mbegu za kutosha, ambapo pia walisema kuna maeneo ambayo hayajafikiwa kabisa, hivyo ni vizuri wananchi wakapelekewa mbegu kwa wakati.

Diwani wa kata ya Masanga Enock Reuben ameuomba uongozi wa bodi ya pamba kuongeza mbegu kwa wananchi kwani mbegu walizogawiwa ni kidogo na wengine wamepelea hawajapata, ambapo baadhi ya watu wanalalamika , ukilinganisha na nyakati hizi zilizopo za uchaguzi wa serikali za mitaa.

"Kwa kweli tunaingia kwenye hali ngumu sana ya lawama kutokana na ugawaji wa mbegu, wananchi wanahitaji kulima pamba kwa wingi, hivyo tunaomba tuongezewe na wengine ambao hawajagawiwa wagawiwe,"amesema Reuben.

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni amesema amesikia taarifa ya mbegu za pamba kwamba hazitoshelezi wakulima,hili lifanyiwe kazi kwa haraka ili kuhakikisha wakulima wanapata mbegu za kutosha.

Aidha ameipongeza halmashauri ya Kishapu kwa ukusanyaji wa mapato, ambapo pia amewataka wahakikishe fedha hiyo inatumika inavyotakiwa, pia amewashauri wajiwekee mikakati ya kuitunza na kusubiri maelekezo yanayotakiwa.

"Naomba niwakumbushe tu wataalamu wote na madiwani mfuatilie miradi ya maendeleo ya halmashauri kuu, isichakachuliwe, kinachotakiwa ni kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zinazotakiwa, pia niwaombe madiwani tushirikiane kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na tuwahamasishe wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura hiyo Novemba 27, 2024"amesema Hamduni.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Emmanuel Johnson amesema maagizo yote yaliyotolewa ameyachukua na suala la mbegu za pamba kuanzia kesho atamuita meneja wa bodi ya pamba ili kuweza kuhakikisha wananchi wanapata mbegu za kutosha waweze kuendelea na kilimo chamba.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya amesema maelekezo haya yaliyotolewa yanatakiwa kufanyiwa kazi, hivyo kwa madiwani na wataalamu bidii zikafanyike ili kuhakikisha halmashauri ya Kishapu inasonga mbele kimaendeleo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Johnson akizungumza kwenye baraza la madiwani
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni akizungumza kwenye baraza la madiwani
Mkuu wa mkoa wa Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye baraza la madiwani Kishapu
Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Piter Mashenji akizungumza kwenye baraza la madiwani
Wataalamu wakiendelea kujibu hoja za madiwani
Mweka hazina wa halmashauri ya Kishapu George Silumbwe akijibu hoja za madiwani
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu Dickson Kamazima akijibu hoja za madiwani katika kikao cha baraza hilo
Afisa kilimo wa halmashauri ya Kishapu Subinus Chaula akijibu hoja za madiwani
Diwani wa kata ya Talaga Richard ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Jamii akitoa taarifa ya kamati yake
Diwani wa kata ya Mwamashele Lukas Nkende ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya uchumi na mazingira akitoa taarifa ya kamati hiyo
Diwani wa kata ya Kishapu Joel Ndetoson akizingumza kwenye kikso hicho
Diwani wa kata ya Mwamalasa Bushi Mpina akizungumza kwenye baraza hilo
Diwani wa kata ya Bubiki James Kasomi akizungumza kwenye baraza hilo
CC wa halmashauri ya Kishapu akisoma ajenda zilizopo
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya, Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Johnson na Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanda CP Salum Hamduni
Kazi ikiendelea kwa wataalamu wa halmashauri ya Kishapu
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiendelea kupokea maelekezo kutoka kwa katibu Tawala wa Mkoa CP Salum Hamduni

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiendelea kupokea maelekezo kutoka kwa katibu Tawala wa Mkoa CP Salum Hamduni
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiendelea kupokea maelekezo kutoka kwa katibu Tawala wa Mkoa CP Salum Hamduni

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiendelea kupokea maelekezo kutoka kwa katibu Tawala wa Mkoa CP Salum Hamduni
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiendelea kufuatilia makablasha yao ili wapate uelewa zaidi
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiendelea kupokea maelekezo kutoka kwa katibu Tawala wa Mkoa CP Salum Hamduni
Kamati ya usalama ya wilaya ya Kishapu ikiendelea kufuatilia ajenda za kikao hicho
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiendelea na baraza hilo

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464