Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamesema wameingiwa na hofu ya ujenzi wa
skimu ya umwagiliaji ya Nyida kutokamilika kwa wakati wakidai ujenzi huo
unakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na mkandarasi anayejenga skimu hiyo
kutoishirikiana serikali ya kijiji na kata katikavi vikao vya taarifa za
maendeleo na kutofanya vikao maalum vya kuuelezea mradi maarufu kama Sight
meeting.
Na mwandishi wetu kutoka Mkoani Shinyanga.
Hali hiyo imejitokeza
baada ya mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga Amos Mshandete kudai ufafanuzi kuhusu mkanganyiko wa taarifa za
ujenzi wa skimu hiyo ya umwagiliaji zinazowasilishwa na wataalamu kwenye vikao kuwa
zimekuwa tofauti na zile zinazofikishwa kwenye kamati hiyo sanjari na kwenye vikao
vya Baraza la Madiwani.
Hata hivyo, diwani wa kata ya Nyida ambako mradi huo unatekelezwa Mh. Selemani Segeleti amekemea tabia ya mkandarasi wa Kichina anayejenga skimu hiyo kutoshirikisha uongozi wa Kijiji na kata na kudai kuwa amekuwa akiwafukuza wasisogelee mradi huo huku Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mh. Nicodemus Simon akimtaka mwanasheria wa halmashauri ya shinyanga kufuatilia jambo hilo kwa karibu na kuleta majibu sahihi kuhusu malalamikoa ya viongozi wa kata ya nyida na madiwani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Ngasa Mboje amemwelekeza Mkurugenzi kuimarisha utendaji kazi wa mifumo ya fedha ili kuepuka miradi ya maendeleo kukwama kutokana na baadhi ya wataalamu wanayousimamia kutokuwa na ufahamu wa kutosha.
Hii ni ripoti ya hali ya skimu ya umwagiliaji ya Nyida ambapo madiwani wanasisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Mkandarasi na serikali ya kijiji na kata ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Baadhi ya picha za ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji ya Nyida halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa katika kikao cha madiwani wa Halmashauri hiyo wakiwasilisha ripoti za utekelezaji wa Miradi ya maendeleo