MAHAFALI YA 4 YA KIDATO CHA NNE LITTLE TREASURES SECONDARY YAFANYIKA

Wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures wakiingia ukumbini kwa kucheza 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures iliyopo Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo, Ijumaa Novemba 29, 2024, na kuwa ni tukio la kihistoria kwa shule hiyo.

Wanafunzi 58, wakiwemo wavulana 28 na wasichana 30, wamehitimu Kidato cha Nne mwaka 2024, huku shule hiyo ikionesha mafanikio makubwa katika maendeleo ya elimu.

Mgeni rasmi katika Mahafali hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa elimu, wazazi, na wanafunzi, yakiwa yamejaa furaha na shangwe alikuwa Saleh Mohamed, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Mohamed ameipongeza shule ya Sekondari Little Treasures kwa maendeleo yake katika elimu na mchango wake mkubwa katika kuinua kiwango cha elimu katika Mkoa wa Shinyanga.

Amesema kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kitaifa, jambo ambalo linaupa heshima mkoa huo.

"Mfumo wa elimu wa shule hii umejikita katika nidhamu, bidii na kujituma, jambo ambalo linawafanya wanafunzi wake kuwa na mafanikio makubwa katika masomo yao," amesema Mohamed.

Aidha, amewasihi wanafunzi waliohitimu kutojihusisha na makundi yasiyofaa, kama vile utumiaji wa dawa za kulevya, akisisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwa na malengo mazuri na kujiepusha na vishawishi vya maovu.

"Ni lazima tuchukue hatua za kutatua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya elimu. Tushirikiane kwa pamoja ili kuendeleza ustawi wa shule na jamii kwa ujumla," ameongeza Mohamed.

Ameuahidi uongozi wa Shule kuwa kiwanda cha Jambo kitakuwa wazi kwa wanafunzi wa shule hiyo kukitembelea ili wapate uzoefu na ujuzi wa kiufundi namna kinavyofanya kazi.
Zoezi la kukata keki likiendelea wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Little Treasures, Alfred Gikaro Nchagwa, amesema shule imeendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kwamba wanafunzi wa Kidato cha Nne mwaka huu wamefundishwa kwa weledi mkubwa ili kukabiliana na mtihani wa taifa (NECTA) na kwamba wanatarajia kupata matokeo mazuri, kama ilivyo kawaida ya shule hiyo.

Meneja wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Wilfred Mwita Nchagwa, amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2018, imeendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu.

Ametoa shukrani kwa wazazi kwa kushirikiana na shule hiyo na kuahidi kuendelea kutoa elimu bora kwa watoto wao.

"Wazazi wamekuwa mabalozi wazuri wa shule yetu, na tunaahidi kuwa tutaendelea kuwaendeleza wanafunzi wetu ili waweze kufikia malengo yao. Tuna ndoto ya kuwa na Little Treasures bora zaidi, na tutahakikisha ndoto za wanafunzi wetu zinatimia," amesema Nchagwa.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Mohono Enoshi, amewashauri wazazi kuleta watoto wao katika shule ya Little Treasures kwa sababu ni shule bora inayozalisha vipaji na kutoa elimu ya kiwango cha juu.

Nao wazazi wa wanafunzi wameishukuru Shule ya Little Treasures kwa kujitolea kwake katika kuwalea na kuwasomesha watoto wao kwa ubora, na kusisitiza kuwa shule hiyo imekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya watoto wao.

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures wakiingia ukumbini kwa kucheza - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures wakiingia ukumbini kwa kucheza
Wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures wakiingia ukumbini kwa kucheza
Mgeni rasmi Saleh Mohamed, akimwakilisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products akitoa hotuba yake kwenye mahafali ya 4 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi Saleh Mohamed, akimwakilisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products akitoa hotuba yake kwenye mahafali ya 4 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Sehemu ya wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Sehemu ya wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Meneja wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Wilfred Mwita Nchagwa akizungumza wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures

Mkuu wa Shule ya Sekondari Little Treasures, Alfred Gikaro Nchagwa akizungumza kwenye mahafali hayo
Keki maalumu wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Zoezi la kukata keki likiendelea wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Zoezi la kukata keki likiendelea wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Zoezi la kulishana keki likiendelea wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Zoezi la kulishana keki likiendelea wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Zoezi la makabidhiano ya zawadi ya keki  likiendelea wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures wakicheza na kutoa zawadi kwa Mkurugenzi wa Shule za Little Treasures Lucy Mwita (hakuwepo)
Wahitimu wakisoma risala wakati wa Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi, Saleh Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi, Saleh Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi, Saleh Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wazazi  waliokuwa wanafuatilia kwa ukaribu zaidi maendeleo ya mtoto katika Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi, Saleh Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi, Saleh Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi, Saleh Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi, Saleh Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Little Treasures
Mgeni rasmi, Saleh Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Little Treasures
Sehemu ya wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures

Sehemu ya wahitimu wa Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Little Treasures

Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali hayo.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464