MGOMBEA wa nafasi ya uenyekiti Mtaa wa Majengo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Issa Mkondo akiomba kura
Na Kareny Masasy, Shinyanga
MGOMBEA wa nafasi ya uenyekiti Mtaa wa Majengo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Issa Mkondo amesema wakimpatia ridhaa ya kuongoza atahakikisha suala la ulinzi na usalama analitekeleza ili wananchi waishi kwa amani.
Mkondo amesema hayo leo tarehe 25,Novemba,2024 katika kufunga kampeni za serikali za mtaa ambapo amesema bila ulinzi na usalama kwa wananchi ni kazi bure.
.
Mkondo ameomba wananchi wamchague pamoja na wajumbe wote ili waweze kuwasimamia na kusikiliza kero zao kwani mhuri utakuwa unakaa ofisini na hawatatozwa gharama yoyote ni mali ya serikali.
Majidi Ally ambaye alikuwa mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo kupitia Chama cha Mapinduzi na sasa ni Meneja Kampeni wa kata hiyo amesema wasichanganye vyama bali wachague Chama Cha Mapinduzi kiwe na maelewano ya kuwaletea maendeleo wananchi.
"Nawaomba msifanya makosa msifunge katika embe la kukokota paka na Ng'ombe kilimo hakitaenda bali wekeni kote kwenye ulinganifu mambo yaende msichague wapinzani hawana sera ya kuwaeleza", amesema Ally.
Katibu wa CCM kata ya Kambarage Hamis Haji amesema utaratibu wa kupiga kura umewekwa vizuri majina yapo na vyama hivyo wasifanye makosa katika upigaji na kuharibu kura.
Mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko akifunga kampeni hizo kwenye mtaa wa Majengo amesema vijana wahamasishane kujitokeza kupiga kura kwani ushindi ni lazima.
MGOMBEA wa nafasi ya uenyekiti Mtaa wa Majengo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Issa Mkondo akiomba kura
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464