Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maebdeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.
Na Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi amemuomba mkuu wa mkoa wa Shinyanga, wakuu wa wilaya Kishapu, Kahama, Shinyanga, vyombo vya usalama na migambo waachie wananchi wachague viongozi wanaowataka.
Hayo wameyasema leo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika kimkoa katika kata ya Masekelo manispaa ya Shinyanga mkoani hapa, ambapo amesema anaviomba vyombo vya usalama viache kuingilia uchaguzi, hivyo waachiwe wananchi wafanye uchaguzi wao kwa haki na amani.
Ntobi amesema ibara ya 3 ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, inasema nchi ya Tanzania ni nchi ya Demokrasia yenye kufuata misingi ya vyama vingi, hivyo ni vizuri jeshi la polisi na wengine wakawaachia wananchi waweze kuchaguaa viongozi wanaowataka wenyewe.
"Nimesema safari hii wananchi msikubali mtu ambaye hajashinda ujumbe au nafasi ya mwenyekiti atangazwe, hivyo tunaomba usimamizi uwe wa haki, tutakubali matokeo kama tutaona uchaguzi umefanyika kwa haki, na ninasema kweli kwa sababu mazonge zonge yameanza toka pale tulipofungua daftari la makazi,"amesema Ntobi.
"Kwani sisi Chadema tulihamasisha wananchi wakajiandikisha kwa wingi lakini wenzetu wakashawishi wanafunzi ambao hawajafikia umri wa kupiga kura ambao walisema uongo kuwa wana umri wa miaka 19 huku wakiwa na umri wa miaka 15 kama tukiruhusu watoto waseme uongo kwa badae tutakuwa na viongozi waongo waongo, ambao watasababisha madhara makubwa kama yaliyotokea juzi Kariakoo", ameongeza Ntobi.
"Niwaombe wazazi wote wa mkoa wa Shinyanga msiruhusu watoto kuja kupiga kura siku ya uchaguzi wakija wao ndio watakuwa kura, pia niwaombe walimu na watendaji mtende haki ili kudumisha amani kama hamtatenda haki amani haitakuwepo siku hiyo,'amesema mwenyekiti wa CHADEMA mkoa Ntobi.
Pia Mwenyekiti Ntobi amewaonya wakuu wa wilaya wote wa mkoa wa Shinyanga waache kuingilia uchaguzi, watendaji, walimu watende haki, watoto wadogo waache kusema uongo pamoja na watu wale wanaojitokeza kupiga kura mara mbili, kwani wakijitokeza wakupiga kura mara mbili watawashughulikia.
"Tutakabiliana nao wale watakaojiandikisha mara mbili tutawashughulikia na lazima tujue kama wewe ni mkazi wa eneo husika, leo tunazindua kampeni hii mpaka jumatano siku ya uchaguzi, hivyo tunahitaji itendeke haki tutakapoona mgombea wetu akishambuliwa shavu la kushoto na sisi hatutakubali tutacheza nao shavu la kulia", amesema Ntobi.
Ntobi aliwaomba wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga wajitokeze kuwapigia kura ili waweze kushinda na kuwatumikia, kwani ilani ya Chama hicho inasema wenyeviti wa mitaa watatoa huduma bure kwa wananchi, watawahudumia wananchi kwa kuwapigia mihuri bure, pia watafuta ushuru wote wa taka.
"Hivyo niwaombe wenyeviti wangu mkawatendee haki wananchi, na mkawaamshe madiwani wafanye kazi kwa nguvu zote kwa ajili ya kufanya maendeleo, hatuwezi kuwa na hospitali ya rufaa bila kuwa na barabara nzuri,kwani kwa sasa hivi tuna barabara ambayo ni Israel mtoa roho, kwani baraba hii ya kuelekea hospitali ya rufaa ni mateso makubwa kwa wagonjwa na kwa wananchi ambao wanaumwa vikohozi kila siku kwa kuvuta vumbi", amesema Ntobi.
Akizungumzia Mikopo ya asilimia 10 amesema vijana wanahitaji mikopo ili wafanye biashara, hivyo wenyeviti wa CHADEMA watashughulikia mikopo hiyo ili kuhakikisha kila kijana anapatiwa mkopo ili kuweza kufanya biashara na kuinua uchumi wa familia na Taifa kiujumla
Kwa upande wake Julius Mwita ambaye alikuwa mgombea wa jimbo la Msoma mjini ambaye alifika katika uzinduzi huo kwa ajili ya kuwatia nguvu, ambaye amezungumzia wanawake wanapoenda hospitali kujifungua wanatozwa fedha hadi za kununua wembe, hivyo amesema wanahitaji serikali ambayo itawajali wananchi na kuwahudumia ipasavyo pindi wanapohitaji huduma za serikali.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maebdeleo Chadema Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Msoma mjini kupitia CHADEMA Julius Mwita akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Msoma mjini Julius Mwita akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa
Wanachama na wananchi wa kata ya Masekelo wakimsikiliza mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi
Wanachama na wananchi wa kata ya Masekelo wakimsikiliza mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi
Wanachama na wananchi wa kata ya Masekelo wakimsikiliza mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi
Wanachama na wananchi wa kata ya Masekelo wakimsikiliza mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi
Wanachama na wananchi wa kata ya Masekelo wakimsikiliza mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi
Wanachama na wananchi wa kata ya Masekelo wakimsikiliza mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi
Wanachama na wananchi wa kata ya Masekelo wakimsikiliza mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464