NGOKOLO WAHITIMISHA KAMPENI KWA KISHINDO KATIKA MTAA WA MAGEUZI NA MWADUI,




Na Suzy Butondo, Shinyangapress blog

Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga kimefanya kampeni zake leo katika mtaa wa Mageuzi na mtaa wa viwanja vya mwadui katika manispaa ya Shinyanga, ambapo kimenadi wenyeviti na wajumbe wake na kuwaomba wananchi wawachague viongozi hao ili kuendeleza maendeleo zaidi.


Wakizungumza kwenye mikutano ya kampeni viongozi mbalimbali wa Chama cha mapinduzi CCM wamesema, chama cha mapinduzi kinachoongozwa na Rais Samia Suluhu wa awamu ya sita kimefanya maendeleo makubwa na kinaendelea kutengeneza barabara katika mitaa mbalimbali katika kata ya Ngokolo na kata zingine ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.


"Niwaombe wananchi wote wa kata ya Ngokolo tuchague viongozi wa CCM ambao watasimamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo, ambao watashirikiana na mwenyekiti wa Taifa Rais Samia pale anapotoa fedha za kufanya maendeleo na wao watasimamia"Amesema Hatibu Mgeja mjumbe wa wazazi Taifa.


Mikutano hiyo ya kampeni imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa CCM wilaya na Mkoa pamoja na wananchi wa kata ya Ngokolo.

Aidha mkutano huo ulihudhuliwa na aliyekuwa mwanachama wa chama cha Maendeleo CHADEMA ambaye alidai kuwa amechoka kulazimishwa kuvuta bange ameamua akihame hicho chama ili apumzike kuvutishwa bange.

"Niseme tu kweli kwamba nimeondoka CCM kwa sababu nimechoka kulazimishwa kuvuta bange, nimeona nihamie CCM ili nikaweze kuwa na amani"amesema Anna Abuolo.























































































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464