ODILIA AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KAMBARAGE,..ENDELEENI KUIAMINI CCM IMEFANYA MAENDELEO MAKUBWA

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza na wananchi wa kata ya Kambarage 

Na Suzy Butondo,Shinyangapress Blog

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo amewataka wananchi wote wa kata ya Kambarage kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi CCM  kwa kuwa viongozi wake wamefanya maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali za kijamii zikiwemo barabara vituo vya afya.

Hayo ameyasema leo wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa  serikali za mitaa uliofanyika leo  Novemba 21,2024 katika mtaa wa majengo kata ya Kambarage manispaa ya Shinyanga mkoani hapa.

Batimayo amesema Chama Cha Mapinduzi CCM  kwa usimamizi mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan kimefanya maendeleo makubwa katika Taifa la Tanzania na kwa kata ya Kambarage, barabara zilikuwa mbovu lakini kwa sasa zinapitika vizuri,kulikuwa hakuna kituo  cha afya lakini kwa sasa kipo na wananchi wanapata huduma vizuri, wanawake wana uhakika wa kujifungua salama, hivyo tuendelee kuzaa tu kwa sababu usalama upo.

"Kinachotakiwa tutembee kifua mbele na tukawe mabalozi wa  kuzungumzia maendeleo  makubwa  yaliyofanyika katika awamu ya sita,hivyo tupo katika kukumbushana na kuwaomba wananchi waendelee kutuamini, kwani mama yetu, mama Samia amefanya maendeleo makubwa na kama kuna mtu ambaye hayaoni maendeleo haya atakuwa na ugonjwa wa afya" amesema Batimayo.

"Na leo kazi kubwa ni kufanya uzinduzi kwa  kuwaomba wananchi wachague wenyeviti na wajumbe wa kutoka CCM na si kwingine kwa sababu maendeleo tunayaona ambayo yalisimamiwa na wenyeviti wa CCM , hivyo tunaomba kura zenu  zote kwa wenyeviti wetu na tunaamini watashinda kwa asilimia 100 , wapinzani waache kufanya majaribio kwenye maendeleo ya watu cha msingi tuchagueni mwenyekiti wa CCM"ameongeza 

 Kwa upande wake diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole amesema toka mwaka 2000 walikuwa na shida ya ufaulu wa watoto, lakini matokeo ya sasa wanafaulu vizuri  na madarasa yapo ya kutosha, wote wataingia darasani hakuna atakayebaki.

Diwani viti maalumu Sheila Mshandete amesema katika kata ya Kambarage wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi kwa kishindo, pia walikuwa na kero ya maji kuingia kwenye makazi ya watu lakini kwa sasa hayaingii tena, viongozi wa CCM wamelishughulikia wananchi wanaishi kwa amani.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464