Wengi tuliofika elimu ya sekondari tumejifunza kwa kiasi maana ya uraia na dhana ya uraia pacha( dual citizenship) na katika nchi yetu Tanzania uraia wa Tanzania unasimamiwa na sheria ya mwaka 1995 sura no 357 na imerekebishwa mwaka 2002 na inaenda sambamba na kanuni uraia ya mwaka 1997.
Sheria imeainisha wazi aina za uraia Tanzania ni tatu
(A)Uraia wa kuzaliwa( citizenship by birth) ( B ) Uraia kwa kurithi ( citizenship by registration)
( C)Uraia wa tajinisi (citizenship by Naturalization)
Kwa mujibu wa haki za binadamu kila mtu yuko huru kufanya maamuzi hasa yanayohusu maisha yake hata kujiamulia wapi pakuishi. Wengi tuna fahamu maana ya liberty as freedom of an individual to live as you wish. Kwa tafsiri fupi ni hali ya uhuru wa mtu kuishi kwa namna anavyoona inafaa .Hivyo mtu kuzaliwa katika taifa flani hakukulazimu kuendelea kuwa raia wa nchi asilia kwa maisha yako yote.
Kupitia dhana hii ya uhuru ndio ina jenga msingi wa kuwa na hili suala la uraia pacha. ama hata kuamua kwa hiari kuwa urai wa nchi yeyote ambayo unaona inafaa kuishi na kujenga familia. Mfano wengi raia wa mataifa hususani ya Afrika wana penda kwenda marekani ama nchi za ughaibuni na hatimaye wengi wanachukua uraia wa nchi hiyo ya Amerika mfano mwana blogger maarufu hapa Tanzania anayefahamika kwa jina la MANGE KIMAMBI ambaye amechukua uraia wa Amerika na sasa ni Mmarekani akifurahia haki za Kimarekani ila asili yake ni uchagani hapa Tanzania
Pia ifahamike wazi kuwa mtu kuamua kuwa raia wa nchi nyingine na kukana uraia wako wa nchi asili sio USALITI bali ni haki ya kiutashi na kutumia uhuru wake.
Sote tunafahamu kuwa hii Dunia ni moja na hii mipaka ya kiutawala imewekwa ili kurahisisha shughuli za utawala na himaya . mfano bara la Afrika liligawanywa mnamo 1885 baada ya mkutano wa Berlin ili kukidhi matakwa ya ma BEBERU walio kuwa wakigombania mali na kukuza himaya zao hapa Afrika (SCRAMBLE AND PARTITION) Hata Geography inaeeleza kuwa dunia yote ili kuwa pande moja la ardhi ila liligawanyika kutokana na nguvu (kani ya mvutano) ya asili na kuzalisha mabara 7 ambayo ukiyaweka pamoja yana kuwa sawa (Gig saw fit evidence)
Vitabu vitakatifu vinabainisha kuwa MUNGU alimuumba ADAM na akaona si vema Adam awe peke yake akatoa ubavu na kumuumba EVA .(ADAM NA HAWA) sasa kama sote ni matokeo ya uzao wa Adam na Eva kwa nini tusiwe huru kuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja na kuwa na haki zote zinazotolewa na nchi hizo. Hivyo uraia pacha ni haki ya asili ya kila binadamu japo inapaswa kuwa na utaratibu mzuri wa kuiweka.
NINI MAANA YA URAI PACHA? Kwa ufupi ni hali ya mtu kuwa raia au mwananchi anayetambulika kisheria na nchi zaidi ya mbili na kuwa na haki zote za kisheria. Tofauti kati ya uraia pacha na diaspora.
DIASPORA ni raia wanao ishi nje ya taifa la asili ila hawajakana utaifa wao ,wanaweza wakawa masomoni, Ama wana fanya shughuli flani hivyo diapora ni wazalendo wa kweli wana manufaa kwa taifa letu ikiwemo kukuza na kueeneza Kiswahili mfano huko nchini China kuna diaspora wengi wana fundisha Kiswahili. Wanaimarisha diplomasia ya kiuchumi (economic diplomacy) kwa kuhamasisha watalii na technolojia. Pia wana tuma fedha kwa ndugu jamaa na marafiki ambapo nchi inapata kodi hivyo wanaongeza pato la taifa na kuongeza makusanyo ya kodi hivyo serikali imeweka mfumo mzuri wa kuwa saidia diaspora kwa kuwapa hadhi maalumu.
HADHI MAALUMU: Kwakuwa suala la uraia pacha limekuwa kizumngumkuti na bado halina muafaka hivyo serikali kwa kutambua umuhimu na mchango wa raia wenye asili ya Tanzania iliamua kwa hiari kuwa raia wa mataifa mengine imekuja na mbadala wa kuwa na hadhi malum ambapo wata kuwa na haki flani ,ikiwemo kuwa na vitamblisho maalum na kufanya uwekezaji hasa ule wa kimkakati mfano kuanzisha viwanda na taasisi zinazoweza kusaidia jamii na nchi kwa ujumla.
Hadhi malumu itasaidia kuongeza pato la taifa kupitia ushuru wa kurudi nyumbani pia itahuisha hali ya kuleta maarifa nyumbani (technological transfer).
Kiukweli nyumbani ni nyumbani hata kama mtu akiukana uraia wa nchi asilia inakuwa tu ili kukidhi vigezo vya kupata uraia wa taifa husika dhumuini ni kuhakikisha maslahi ya mhusika yanafikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi husika lakini moyo na dhamira inabaki kuwa kwenye taifa la asili,hivyo hadhi maalum kwa wale walio chukua uraia wa nchi nyingine ni kitu cha kupongezwa. Ni sawa na mtu ambaye ameweka makazi yake mjini lakini kila siku anawasiliana na watu wa nyumbani hiyo tunaita home umbirical ties. Hivyo hadhi maalumu ni mkakati mzuri wa kuwatumia hawa walio na uraia wa nchi hizo kwa maslahi ya taifa letu.
KWANINI URAIA PACHA NI HATARI KWA USALAMA WA TAIFA LETU
Kwa mujibu wa somo la uraia (civics) Taifa lina undwa na vitu vii nne(components of Nation)
Watu (population)
Eneo la kiutawala(territory)
Mamlaka kamili ya kujitawala(sovereignity)
Kutambuliwa kimataifa(international recognition)
Hivyo watu ni kitu muhimu sana kwa taifa lolote na watu hawa lazma waweze kuwa watiifu kwa mamlaka na utawala wa Taifa husika yani soverenity of the state sasa ni vigumu sana kwa mtu kujigawanya kuwa mtiifu kwa mamlaka mbili.
Sheria ya uraia ya Tanzania kifungu namba 357 ya mwaka 1995 inasema “Wote waliokana uraia wa Tanzania watapoteza haki ya kuendelea kuwa raia wa Tanzania”
Kama mtu akiwa na akili timamu bila kushinikizwa na yeyote akaamua kuukana uraia wa Taifa lake ni mtu wa kumuangalia kwa jicho la pekee sana. na sheria imeweka wazi kabisa ukiukana uraia na kuwa raia wa nchi nyingine utakuwa umepoteza haki zote za kuwa Tanzania.
Hii sheria iko sawa sana ikiwa na dhumuni la kulinda usalama wa nchi yetu na heshima ya Taifa huru linalojitawala bila kuingiliwa na taifa jingine(as sovereign state)
Kwa mujibu wa Profesa KABUDI PALLAMAGAMBA akiwa bungeni alisema kuwa utafiti alioufanya unaonyesha 51% ya nchi duniani hazijaruhusu uraia pacha.
HATARI ZA URAIA PACHA KWA TAIFA
Una punguza uzalendo kwa Taifa la asili. Uzalendo ni hari ama hurka ya mtu kulipenda taifa lake kujitolea kulilinda na kulitetea katika mazingira mazuri na magumu mfano wakati wa vita wazalendo hupigana ili kulinda Taifa kwa hapa Tanzania mwaka 1978 tukiwa vitani zidi ya Nduli Amini Dada. Wazalendo walijitoa kulinda na kulitetea Taifa sasa kukiwa na raia wana uraia wa nchi mbili au zaidi kiuhalisia huwezi simama na taifa na kulilinda na kulitetea. Hata historia inaonyesha 1938 huko Ujerumani wa jewish waliamriwa kuondoka na walipokwa haki zote ikiaminika kuwa ni wasaliti wa taifa la ugerumani wakati wa vita vya pili vya dunia. Kwa msingi huo uraia pacha ni hatari sana kwa usalama wa nchi yetu. Watu tuwe wazalendo tulipende taifa letu tujitoe.
2..Unaondoa dhana ya utiifu kwa mamlaka ya nchi (Obedience to states sovereignity au loyality) ili mtu uwe mtiifu ni lazima uwe na mamlaka moja unayo itii hata kwenye Biblia imenenwa you can’t save two masters at once yaani huwezi watumikia mabwana wawili kwa pamoja. Kwenye hili ni dhahiri shairi kwamba mtu mmoja hawezi tii mamlaka za mataifa mawili kwa pamoja. Mfano raia mmoja mchezaji au msakata kabumbu anatakiwa na team ya taifa lake kuchezea team ya taifa kwa muda huo huo ana inaitajika na taifa jingine atajigawaje ili kutimiza wajibu huo kwa mataifa mawili kwa pamoja at once? Jibu ni kizungumkuti sasa nadhani uraia pacha unahatarisha hata maslahi ya nchi hivyo sheria yetu iko vizuri na iendelee kusimamiwa kama ilivyotungwa.
3..Inaondoa hadhi ya utaifa ama utambulisho wa taifa ( National hood or Natinal identity) ni muhimu kujivunia kuwa na hadhi ya taifa moja sasa mtuu akiwa na uraia wa zaidi ya mataifa mawili akiiitaji kuji tambulisha ataijitambulisha kama raia wa nchi gani? Hata historia ina onyesha miaka ya 1880 kipindi cha ukoloni Taifa la Ufaransa likiwa na sera yake ya Assimilation policy wote waliokidhi vigezo walipewa kuwa raia wa Ufaransa wakiacha kuwa raia wa mataifa yao. Hii ni kukuza utaifa.na hata utamaduni wa taifa la asili una dhoofikaa kwa mtu kuwa na uraia wa nchi Zaidi ya moja. Hivyo tuendelee kusimamia sheria yetu inayolinda utaifa wetu.
4…Unahatarishaa siri za taifa na desturi ya taifa. Katika kila taifa kuna mambo ya wazi kwa maslai mapamna ya taifa na kuna idara nyeti za nchi zinaitajika kuongozwa na wazalendo wa kweli. Sasa uraia pacha unaweza sukumwa nahii dhana ya haki zabinadamu ikapelekea watu wenye uraia wa nchi mbili kufanya kazi katika vitengo nyeti mfano IKULU. Sasa hiyo kiuhalisia lazima ina weza vujisha siri za taifa kwa mataifa mengine ambayo hayana nia njema na taifa letu. Kwa msingi huo nimuhimu kueendelea na huu utaratibu wa kuto ruhusu urai pacha hapa Tanzania.Pia hata raia ambao hawana asili ya Tanzania nao we have to be kin Kwa kuwa umbirical ties bado inaweza toa msukumo kwa siri za Taifa.Kwa hili tutoe pongezi kwa Viongozi wetu wakati wa ujenzi wa IKULU CHAMWINO walitumia wazalendo pekee kujenga majengo hayo maalum ya Taifa. Hivyo tuendelee na huu msimamo na sheria hii ni nzuri na ni ya kizalendo.
5. Unaondoa umoja wa kitaifa (Natinal unity and solidarity) Taifa letu nitaifa la kijamaa ambalo lili asisi hii falsafa 1967 katika azimio la Arusha ambalo linaamini kuwa bina damu wote nisawa na kila mmoja astahili heshima na kuthaminiwa utu wake . Na hii itikadi inadumu kwakuwa rai wa Tanzania wote tuko katika huu mwamvuli wa umoja na mshikamano na hii ideilojia itadhoofika endapo tuta ruhusu watu kuwa na uraia pacha ambao hawatakuwa na morali ya kuenzi tunu hii muhimu ya Taifa
6.. Inaondoa utambulisho wa taifa ikiwemo lugha. Taifa letu lina utambulisho wa Kiswahili kuwa lugha ya taifa na tuna jivunia na kuitambulisha dunia kuwa Tanzania ndio chimbuko la lugha hii adhimu ya Kiswahili na ni tamaduni pia sasa tukiruhusu uraia wa pacha hao kama wameweza kuukana uraia je? Kuhusu lugha watajivunia kweli? Hapa ni kuzuia huu uraia pacha kwa nguvu zote na jitihada zote
7.Unakanganya mfumo wa mashtaka kwa wale wenye makosa ya jinai (it compromises judicial extradition or persecution) ikitokea mtu mwenye uraia pacha akawa ametenda makosa ya kijinai na akakimbia taifa moja na kwenda taifa jingine atahukumiwaje? Ili kuepukana na hili ni muhimu kuendelea kuukataa uraia pacha.
HITIMISHO
Kwa kuhitimisha uraia pacha hauna maslahi na faida kwa nchi ya asili zaidi sana ni maslahi ya mhusika tu ili akidhi vigezo vya kufikia matamanio yake ama malengo yake na sio malengo ya Taifa.
Malengo ya nchi yetu ni kuona Taifa hili linaendelea kuwa moja na linadumisha misingi na miiko ya kihistoria na kuenzi MUUNGANO WETU .
MAKALA HII IMEANDIKWA NA
JOHN FRANCIS HAULE
;MKUU WA SOKO KUU LA ARUSHA. (MARKET MASTER)
0756717987 AU 0711993907
EMAIL.haulej4@yahoo.com or haulej46@gmail.com