UBALOZI WA SWEDENI-WATOA WITO MIFUMO YA USALAMA WANAHABARI TANZANIA

 UBALOZI WA SWEDENI-WATOA WITO MIFUMO YA USALAMA WANAHABARI TANZANIA



Na kareny Masasy.

MWAKILISHI  kutoka ubalozi wa Sweden na mratibu wa wa shirika la Maendeleo la Sweden (Sweden International Development Agency-SIDA). Stephen  Chimalo amesema wanataka  uwepo  mfumo mzuri  ambao unaweza   kujengwa kwa kupitia wadau na serikali  kwa kuhakikisha waandishi  wa habari wanakuwa kwenye mazingira yaliyosalama.

Chimalo amesema hayo leo tarehe 2, Novemba.2024 Katika maadhimisho ya  siku ya  kupinga dhuluma na Ukatili dhidi ya waandishi wa Habari ambapo amesema waandishi wa habari wamekuwa wakishindwa kufanya  vizuri kuripoti  kero na changamoto kutokana na kukosa ulinzi.

“Mwandishi wa habari anapotaka kufanya kazi yake ahakikishiwe usalama wake  wa kimazingira  na kiafya na sio Tanzania pekee hata nchi  nyingine waandishi wanahatarishiwa usalama wao hivyo tunataka uwepo mifumo mzuri  ambayo  inaweza  kujengwa kwa kupitia wadau na serikali  kwa kuhakikisha waandishi wanakuwa kwenye mazingira yaliyosalama”amesema Chimalo.

Chimalo amesema kuna  mwandishi  mmoja wa kike kutoka mkoani  Manyara alikuwa anafanya utafiti  kuhusu wadada wanao jiuza nyakati za usiku alijiuliza   katika usalama wa mwandishi huyu  pia mwingine alikuwa anataka kuripoti habari kuhusu mtoto mchanga kutupwa lakini  wanakijiji walidai asiandike  hiyo ni changamoto.

“Napenda kuwashukuru  UTPC  na IMS  kuhakikisha wanatekeleza jambo la usalama kwa waandishi na kujenga usalama kati ya jeshi la polisi na Waandishi wa habari  kwa juhudi wanazozifanya  ikiwemo kuwalinda na kuwathamamini waandishi wa habari”amesema Chimalo.

Chimalo amesema   Shirika la  Umoja wa  Mataifa Elimu,Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) imeanza kufanya mchakato na  Mfuko wa taifa wa bima ya Afya  (NHIF )kuhakikisha waandishi wa habari wanapata bima za afya  lengo kuwahakikishia usalama wao kiafya.

Tunaweza kuwashawishi zaidi  kusaidia waandishi kupata bima za afya,usalama wa waandishi pamoja na kupata kipato, ukiwa na uhakika wa mapato  hata uhakika wa kule unakoenda kutafuta habari unakuwa na usalama  na hili ni kipaumbele  sababu ya usalama wa waandishi”Chimalo.

Siku hii ni kubwa kwetu  kutokana na siku hii ambapo  waandishi wawili wa Ufaransa waliuwawa na kupelekea tarehe 2 Novemba  iwe inaadhimishwa lengo kukumbusha uwajibikaji kwa serikali kuhakikisha  uwepo wa Usalama wa Waandishi.

Rais wa Umoja wa Klabu za  Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema   katika kipindi  Cha mwaka  2024 ambapo UTPC wamerekodi jumla ya matukio 14 yakihusisha waandishi wa habari 26 Kati ya hao 21 ni Wanaume na watano ni  wanawake.

"Wahusika wa matukio hayo ya ukiukwaji wa haki za waandishi  wa habari  wamekuwa wakiachwa  bila kuchukuliwa  hatua ,ukosefu  huu wa uwajibikaji  wa adhabu imejenga mazingira ya hofu  na kujidhibiti  hali hii imedhoofisha uwezo wa vyombo  vya habari  kufanyakazi  kwa Uhuru na hivyo kudidimiza demokrasia"amesema Nsokolo.

Edwin  Soko akiwasilisha  mada inayohusu  Impunity and Impact to Journalism in Tanzania  amesema   madhila kwa  waandishi wa habari  hapa nchini  kuanzia Januari  hadi sasa   vipo visa mkasa 22  ambavyo  vimekwisha tokea hivyo  wasipuuze katika ulinzi na usalama wao.

 “ Kwa mujibu wa Shirika la  UNESCO  limetoa takwimu  kwa mwaka 2022  kuwa hapa duniani  hasa kwenye nchi zinazoendelea na vita na migogoro  waandishi 28 walipoteza maisha  na mwaka 2023  waandishi wa habari 38  walipoteza Maisha na mwaka huu takwimu bado  haijatolewa hali itakuwaje inaweza pia kuongezeka “amesema Soko.

“Sasa hivi Mitandao ya kijamii inachukua  nafasi k ubwa katika vyombo vya habari vingine ambapo vyombo hivyo kumejengeka hofu na woga  na matokeo ya  kubadilisha maudhui  na jamii kuanza kukosa uaminifu kupitia vyombo hivyo”amesema Soko.












Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa klabu za Habari Tanzania wakifatilia shughuli za mkutano









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464