Wenyeviti wa vyama
vya msingi vya ushirika Wilayani Kishapu wamelalamikia vyama vyao kulipwa
ushuru mdogo na usiokidhi mahitaji wakati wa msimu wa ununuzi wa zao la pamba
wakidai kuwa ushuru huo umekuwa ukipannda na kushuka kila mwaka bila kujali ugumu
wa shughuli za ukushanyaji wa zaola pamba kutoka kwa wakulima hali
inayosababisha vyama vingi kupata hasara na kushindwa kuendeleza shughuli za
ushirika
Na Mwandishi wetu kutoa Mkoani Shinyanga.
Malalamiko ya
viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika wilayani Kishapu yameibuka Katikati
ya mkutano wa viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) yakilenga
kufikisha ujumbe kwa viongozi wa serikali Pamoja na viongozi wa SHIRECU na Bodi
ya Pamba Tanzania TCB
Afisa ushirika wa Wilaya
ya Kishapu Bwana Faraji Kimwaga amekiri kuwa changamoto hizo anazifahamu na
kuunga mkono viongozi hao kudai marekebisho ya changamoto mbalimbali wanazozilalamikia
ikiwemo ushuru mdogo na malipo mengine pungufu.Kwa upande mwingine
Meneja wa SHIRECU Kanda ya Mhunze Bwana Ramadhan Kato amekubaliana na umuhimu
wa malalamiko hayo kuyafikisha panapohusika ili kutatua kero na changamoto
zinazoonekana kuanza kukwamisha Ushirika wilayani Kishapu na Mkoa wa Shinyanga
kwa ujumla.Kutokana na hali hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bwana Joseph Mkude ameagiza kuitishwa mkutano maalum
kitakachowashirikisha viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika, viongozi wa
Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU)na Bodi ya Pamba (TCB) ili kujadili
changamoto hizo.Imeelezwa kuwa hii ni
hatua muhimu katika kuhakikisha vyama vya msingi vya ushirika vinaweza kufanya
kazi kwa ufanisi zaidi bila kuwa na vikwazo vya kifedha ambavyo kwa miaka mingi
vimekuwa vikididimiza shughuli za vyama vya ushirika nchini.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464