WANAOCHOCHEA VITENDO VYA RUSHWA KIPINDI CHA UCHAGUZI NI WALE WAGOMBEA WANAOJITOA,MACHAWA NA UNATUACHAJE



Mkuu  wa Takukuru wilayani Kahama  mkoani Shinyanga   Abdalah Ruari.

Na Kareny  Masasy,Kahama

TAASISI  ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru)  wilayani Kahama mkoani Shinyanga   imewaonya wagombea waliopitishwa na  kujitoa   na machawa  katika uchaguzi  mkuu na serikali za mitaa  ndiyo wanaohusika na vitendo vya rushwa.

Pia wanaodai unatuachaje nao wanakuwa ni miongoni wanaoshawishi mgombea  kutoa rushwa hilo ni kosa nani vitendo  vinavyojitokeza katika chaguzi za kuanzia serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao.

  Ofisa wa Takukuru  kutoka  wilayani hapo  Mlamuzi  Kuhanda  ambaye ni  mchunguzi  wa Masuala ya  rushwa amesema hayo  leo tarehe 11,Novemba,2024  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari  kuhusu mwelekeo wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kuhanda amesema  rushwa ni kosa la maadili  nani kosa la kiimani  na sasa kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa   hali ambayo  inakuwa na  vitendo vya rushwa  inapaswa ukemewa kwa nguvu zote hasa  wanaotoa ushawishi kwa njia ya pesa,vitenge, Sabuni au tisheti.

Kuhanda amesema   Uchaguzi huu ni muhimu kwani ni dira ambayo inaonyesha muelekeo wa uchaguzi ujao na viongozi wazuri  kwani  ikitolewa rushwa ni  sawa na  zambi yoyote iliyopo hapa  duniani.

 “Ipo haja ya kuibadilisha jamii  kwa  mtazamo wa kumuangalia mla rushwa kuwa ni shujaa na mtazamo uwe mla rushwa  ni mwenye zambi”amesema   Kuhanda.

Kuhanda alisema kwa mujibu wa    Shirika la  National Government  Social and  corrupition Survey   na   Shirika la Internationa Economic Survey yalifanya  uchunguzi  mwaka 2020  nakubaini  kuwa  asilimia 42.7 waliohojiwa   walidai wanao anzisha vitendo vya rushwa ni watoa huduma.

Kuhanda amesema  asilimia 27.2   waliohojiwa walidai wanaoanzisha  ni wale huhitaji huduma  wanatoa rushwa  na  asilimia 23.5 waliohojiwa watoa huduma na wanaohitaji huduma wote walijihusisha na rushwa.

Mkuu  wa Takukuru wilayani Kahama Abdalah  Urari  amesema    waandishi wa habari na  Takukuru  wanalojukumu la kuweka mikakati ya pamoja  kuzuia rushwa  kwa mujibu wa  ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inavyoelekeza.

“Kutambua  rushwa  ni adui wa Maendeleo Ibara ya tisa (S)  ya katiba hiyo hiyo  inaelekeza kwamba mamlaka ya nchi na taasisi zake  inahakikisha  juhudi zote. zinatokomeza rushwa nchini”amesema Urari.

Ofisa kutoka Takukuru   Happnes Bilakwate amesema wananchi wanatakiwa kupitia na kusoma  mitandao ya kijamii ya taasisi hiyo ili kujua sheria na vitendo vinavyokatazwa juu ya kupinga vitendo vya  rushwa hapa nchini.

"kupitia wadau wetu wa habari mtusaidie kuhamasisha wananchi  wafuatilie page ya taasisi kwenye mitandao ya kijamii kama insta,facebook,twiter  na uifuate na kubscribe you tube channel ya Takukuru Tv  ili kupata habari mbalibali za masuala ya rushwa"amesema Bilakwate.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464