AMREF HEALTH AFRICA TANZANIA YAKABIDHI MAGARI SITA OR - TAMISEMI KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA MIKOA YA MARA NA SIMIYU



Sehemu ya Magari yaliyotolewa na Amref Health Africa Tanzania kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya katika mikoa ya Mara na Simiyu
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt. Grace Magembe amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa ya Mara na Simiyu kuyatunza magari wanayokabidhiwa ili yaendelee kuwahudumia wananchi katika eneo la afya kwa muda mrefu zaidi.

Dkt.  Grace ameyasema hayo katika zoezi la kukabidhi magari mawili kwa Makatibu Tawala waliowakilishwa na Waganga Wakuu wa Mikoa hiyo yaliotolewa na Taasisi ya Amref Health Africa Tanzania kwaajili ya usimamizi shirikishi wa shughuli za Afya katika Mikoa hiyo katika viwanja vya TAMISEMI jijini Dodoma tarehe 11.12.2024.

“Magari haya yanapokabidhiwa kwetu tunaowajibu wa kuendelea kuyatunza na kuhakikisha yataendelea kufanya kazi vizuri ili kuhudumia wananchi”,amesema Dkt. Grace.

Aidha Dkt. Grace ameendelea kupongeza ushirikiano uliopo kati ya Serikali na Wadau mbalimbali wakiwemo Amref Health Africa Tanzania kwa namna wamekuwa wakisaidia katika kutoa huduma mbalimbali za Afya kwa wananchi. 

Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Health Africa Tanzania ,Dkt. Frolence Temu
amesema jumla ya magari yaliyotolewa na taasisi hiyo ni sita ambapo kila mkoa unapata magari matatu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464