DC DODOMA ATAHADHARISHA UPOTOSHAJI WA MAUDHUI MTANDAONI-MKUTANO MKUU WA MISA-TAN

DC DODOMA ATAHADHARISHA UPOTOSHAJI WA MAUDHUI MTANDAONI-MKUTANO MKUU WA MISA-TAN

Na Marco Maduhu,DODOMA

MKUU wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri, amewatahadharisha waandishi wa habari, pamoja na watumiaji wengine wa mitandao, kwamba wanaposambaza maudhui yao mitandaoni, wakumbuke kwamba sheria zipo, na wasiitumie vibaya kufanya upotoshaji.
Amebainisha hayo leo decemba 4,2024, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (Misa-Tan)Tawi la Tanzania,ambao unafanyika Dodoma katika ofisi za jengo la mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF),unaoambatana na mafunzo ya kujadili maudhui potofu ya mtandaoni, pamoja na uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa Taasisi hiyo.

Amesema watu ambao wanatumia mitandao vibaya wakiwamo na waandishi wa habari,wakumbuke kwamba sheria zipo za maudhui ya mtandaoni,hivyo wanapaswa kuwa makini katika usambazaji wa maudhui yao kwa kutopotosha sababu watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“tunapaswa kuwa wazalendo na nchi yetu,na tuitumie vizuri mitandao namna ya kuripoti taarifa, tusipotoshe umma, taarifa zikiandikwa ndivyo sivyo kunaweza kuleta machafuko katika nchi yetu,”amesema Jabir.

“Tumemaliza uchaguzi wa serikali za mitaa, mwakani ni uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani, hivyo tuitumie vyema mitandao kutoa elimu kwa wananchi juu ya uchaguzi huo kwa kuwapatia taarifa mbalimbali kwa kushirikiana na Mamlaka husika ikiwamo Tume ya uchaguzi,”ameongeza.
Aidha, amewasihi pia waandishi wa habari kwamba wawe na wivu na taaluma yao, pamoja na kutokubali kutumika,pamoja na kutoa elimu na kukemea watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao vibaya na kuichafua taaluma hiyo.

Katika hatua nyingine, ameipongeza Misa-Tan kwa kusimamia Katiba yao pamoja na kufanya Mkutano Mkuu, na kueleza kwamba taasisi ambazo haifanyi mikutano haweziwe kusimama imara, huku akiitakia uchaguzi mwema wa viongozi wao wapya.
Naye Mwenyekiti wa Misa-Tan Salome Kitomari ambaye amemaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba ya Misa, akizungumza wakati akimkaribisha mgeni Rasmi, amesema kwa sasa ulimwengu upo kwenye Teknolojia kubwa ya kimtandao pamoja na matumizi ya akiri mnemba na hivyo kusababisha kuwapo na habari nyingi za upotoshaji.

“kwa sasa tupo kwenye dunia ya mitandao ambayo ina mambo mengi, pamoja na matumizi ya akiri mmemba na kumekuwa na habari nyingi za upotoshaji, ndiyo maana tunafanya mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wa habari,ili tuwe makini na matumizi ya mitandao na akiri mmemba, na wasitoe maudhui ya upotoshaji,”amesema Salome.
Mkurugenzi wa uendeshaji kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF)Mhandisi Albert Richard, akiwasilisha mada kuhusu mradi wa ujenzi wa Minara 758, amesema mpaka sasa imesha washwa Minara 306 ambayo itanufaisha wananchi milioni 8.5.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN leo Jumatano, Novemba 4, 2024 katika ukumbi wa UCSAF Jijini Dodoma - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN

Mwenyekiti wa MISA TAN, Salome Kitomari akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN

Mkurugenzi wa MISA TAN, Elizabeth Riziki akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN
Mkurugenzi wa MISA TAN, Elizabeth Riziki akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri na washiriki wa Mkutano wa MISA TAN wakipiga picha ya pamoja
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri na washiriki wa Mkutano wa MISA TAN wakipiga picha ya pamoja

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464