Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amehitimisha ziara yake Wilaya ya Shinyanga Mjini, kwa kufanya Mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya stand ya zamani, ambapo amezungumza na maelfu ya wananchi wa Shinyanga.
Mabala amewashukuru wananchi wa Shinyanga kwa kuendelea kukiamini chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwachagua Wenyeviti na Wajumbe wao waliotokana na chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika tarehe 27 November 2024.
Mabala amesema hawakufanya makosa na kuwaahidi watengemee kufanyiwa kazi vizuri.
Pia amewashukuru wanachama wa vyama rafiki kwa kukipigia kura chama Cha Mapinduzi (CCM) na kubainisha kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Pia amewashukuru Wapinzani kwa kusimamisha wagombea maana bila wao pasingekuwa na uchaguzi na bila wao "tungetangazwa vipi?"
*Mabala* ,amesema kushukuru nikuomba tena ametumia hadhara hiyo kuwaomba wananchi wa Shinyanga mwakani 2025 kwenye uchaguzi Mkuu waendelee kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwachagua Madiwani, Wabunge na *Mhe Rais Samia Suluhu Hassan*, Mama wa Watanzania kwa kura nyingi za kishindo. Kwani maendeleo yamemwagika Shinyanga.
Kila mahali kuna mkono wa mama
Badae Mabala alifanya mkutano wa ndani katika ukumbi wa Shy kom. Nakuwafunda wenyeviti wa Serikali za mitaa na vijiji pamoja na vitongoji na Wajumbe.
Ili waende wakawatumikie wananchi vizuri bila kuwabagua.
Imetolewa na :-
Ndugu Richard Raphael Masele
Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Shinyanga
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464