WAZIRI WA UJENZI ABDALLAH ULEGA AUNGANA NA WANANCHI KUMUOMBEA DUA RAIS SAMIA


Waziri wa Ujenzi na mbunge wa Mkuranga, Mh. Abdallah Ulega ameungana na wananchi wa wilaya hiyo, kufanya dua maalumu ya kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake na kuliombea Taifa ili liwe na amani, umoja na mshikamano utakaowezesha maendeleo endelevu.

Dua hiyo imefanyika Jumamosi Disemba 14 katika uwanja wa Shule Msingi Mkuranga mkoani Pwani ambapo ilihudhuriwa na Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri na maelfu ya wananchi kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo.

Kabla ya dua hiyo ilitanguliwa na Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika asubuhi yaliyowakutanisha masheikh mbalimbali waandamizi wakiwemo wa mikoa ya Arusha, Kigoma, Kagera, Dar es Salaam na Pwani.

Katika dua hiyo ujumbe mkubwa uliotawala ni amania mbapo Watanzania wamesisitiziwa kuitunza ili kuunga mkono jitahada za Dk Rais Samia ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa mstari wa mbele kuhubiri amani.

Mbali hilo, suala la maadili lilisisitiziwa kwa kiwango kikubwa kwa kuelezwa kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anatunza na kuyalinda maadili kwa manufaa ya Taifa.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464