JAMBO YASAMBAZA UPENDO “SELEBRETIKA KIJAMUKAYA”KWA KUGAWA VINYWAJI KWA WAGONJWA KITUO CHA AFYA KAMBARAGE
Kampuni ya jambo group, imetoa zawadi ya vinywaji zenye chapa ya Selebretika kijamukaya,kwa wagonjwa katika kituo cha afya kambarage manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kuleta furaha kwa wateja na watumiaji wa bidhaa za jambo katika msimu wa sikukuu.
Zawadi hizo zimetolewa leo Desemba 22,2024.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George, ambaye pia ni kiongozi wa ubunifu na msimamizi wa chapa jambo group, amesema katika uzinduzi wa kampeni ya selebretika kijamukaya, ni maalumu kwa watumiaji wote wa bidhaa za jambo kufurahia msimu mzima wa sikukuu, kwa kutumia vinywaji vya kampuni hiyo.
Amesema katika muendelezo wa kuleta furaha majumbani kwa kutumia bidhaa za jambo siku ya sikukuu, hivyo wameamua kuwakumbuka wateja wao ambao wapo hospitalini kwa kuwapelekea vinywaji pamoja na biskuti zikiwa na chapa ya selebretika kijamukaya, ili wafurahie msimu mzima wa sikukuu na bidhaa za jambo, sababu ni bidhaa zilizotengenezwa kwa ubora.
“Mwenyekiti wa kampuni za jambo Salum Hamis hakuanzisha kampuni hizi kwa ajili ya kupata faida tu,bali ni kugusa pia maisha ya watu,na ndiyo maana leo tumeamua kuleta furaha kwa wagonjwa na watumishi wa kituo hiki cha Afya Kambarage, kwa kuwapatia vinywaji na biskuti zenye chapa ya selebretika kijamukaya kwa ajili ya kufurahia msimu wa sikukuu,”amesema George.
Pia, amesema baadhi ya vinywaji wataviacha kwenye benki ya damu, na kwamba wananchi ambao watafika kutoa damu watapewa vinywaji hivyo vya jambo, na kuwa sehemu ya mchango wao katika kuokoa uhai.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage Dk. Ernest Magula, ameipongeza Kampuni hiyo ya jambo, na kwamba zawadi hizo za vinywaji na biskuti ni faraja kwa wagonjwa.
Amesema vinywaji vingine vitasaidia kwenye benki ya damu,huku akitoa wito kwa wananchi na vikundi mbalimbali, wajitokeza kujitolea damu sababu uhitaji wa damu ni mkubwa katika kituo hicho.
Baadhi ya wagonjwa katika wodi ya wazazi akiwamo Selina Shija, wameshukuru kupewa zawadi hizo, na kwamba wao ni wateja wa zuri wa kutumia bidhaa za jambo, na kuipongeza kampuni hiyo kuwakumbuka wateja wao hadi sehemu za huduma za Afya, na kuwapatia faraja.
Aidha, jana kampuni ya jambo group ilizindua kampeni ya Selebretika kijamukaya na bidhaa za jambo msimu wa sikukuu,kwa ajili ya wateja wao na watumiaji wote wa bidhaa za kampuni hiyo, kufurahia vinywaji vya jambo vikiwa na chapa ya “selebretika kijamukaya” maalumu kwa ajili ya msimu mzima wa sikukuu,ili watu wafurahie na familia zao.
TAZAMA PICHA👇👇
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George,ambaye pia ni kiongozi wa ubunifu na msimamizi wa chapa jambo group, wapili (kutoka kulia) akimkabidhi vinywaji na biskuti Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage Ernest Magalu.
Wagonjwa katika wodi ya wazazi wakiendelea kupewa zawadi ya vinywaji vya jambo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464