Ndege zimetua uwanja wa Ibadakuli Shinyanga
NDEGE za dharura zimeelezwa kutua katika uwanja wa ndege Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga,na kwamba uwanja huo kwa nyakati za mchana ndege zinaweza kutua,na ujenzi wake umekamilika asilimia 80.
Hayo yamebainishwa leo Desemba 23,2024 na Mhandisi Ruburi Kahatano kutoka Kampuni ya Chico, ambao ndiyo wanajenga uwanja huo, wakati wa ziara ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga,walipotembelea kuona maendeleo ya upanuzi wa ujenzi wa uwanja huo wa ndege Shinyanga.
Amesema uwanja huo asilimia kubwa umekamilika, na kwamba kuna ndege mbili za dharura zimeshatua, ambapo moja ili kutua kwa ajili ya kubeba Mgonjwa kumpeleka hospitali ya Mlonganzila Dar es Salaam kwa matibabu zaidi ya kibingwa na kuokoa maisha yake.
“Uwanja huu kwa ndege za mchana zinaweza kutua, lakini usiku haziweze sababu bado hatujafunga taa,”amesema Mhandisi Kahatano.
Mhandisi Chiyando Matoke kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)Mkoa wa Shinyanga, ambao ndiyo wasimamizi wa ujenzi wa uwanja huo, amesema ulianza kujengwa Aprili mwaka jana, na unatarajiwa kukamilika Aprili mwakani, kwa gharama ya sh.bilioni 44.8 bila VAT, na kwamba umekamilika kwa asilimia 80.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, amesema katika ziara hiyo, wameshuhudia kazi kubwa ambayo inafanywa na serikali, juu ya ujenzi wa miradi ya kimkakati.
Amesema kukamilika kwa uwanja huo wa ndege, utafungua fursa za kiuchumi katika mkoa wa Shinyanga.
TAZAMA PICHA👇👇
Mhandisi Chiyando Matoke kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)Mkoa wa Shinyanga akielezea maendeleo ya upanuzi ujenzi uwanja wa ndege Shinyanga.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza katika ziara hiyo.
Meneja mradi wa upanuzi ujenzi wa uwanja wa ndege Shinyanga Shi Yinlei kutoka Kampuni ya Chico akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mhandisi wa ujenzi wa upanuzi uwanja wa ndege Shinyanga Ruburi Kahatano akizungumza kwenye ziara hiyo.
Waandishi wa habari Shinyanga wakiendelea na ziara katika uwanja wa ndege Shinyanga.
Barabara ya kurukia na kutua ndege (Runway) ikiwa imekamilika kwa asilimia 100.
Barabara ya kurukia na kutua ndege (Runway)ikiwa imekamilika kwa asilimia 100.
Ziara ikiendelea.
Jengo la abiria likiendelea kujengwa.
Ziara ikiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa katika uwanja wa ndege Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464