RAIS SAMIA ATOA ZAWADI YA CHAKULA SIKUKUU YA MWAKA MPYA KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU WILAYANI KISHAPU
RAIS Samia Suluhu Hassan,ametoa zawadi ya chakula na vitu mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu wilayani Kishapu, ili kusheherekea vizuri sikukuu ya mwaka mpya 2025.
Zawadi hizo zimetolewa leo Desemba 29,2024, na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mboni Mhita, ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Mboni amesema, Rais Samia ana upendo na watu wenye mahitaji maalumu,ndiyo maana amekuwa akitatua changamoto zao mbalimbali ambazo huwakabili, na katika sikukuu hii ya mwaka mpya, ameamua kutoa tabasamu kwao na kuwapatia zawadi ya chakula, ili wafurahie na familia zao.
“Vyakula ambavyo nakabidhi leo ni mchele, sukari,mafuta ya kupikia, unga wa sembe,ngano,viungo vya pilau, sukari, mbuzi, vitu vingine ni mafuta ya kupata,’pampers’ za watoto pamoja na juisi,”amesema Mboni.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed, amesema zawadi hizo ni faraja kubwa kwa watu wenye mahitaji maalumu, na kumpongeza Rais Samia kuwa na moyo wake wa upendo.
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu wilayani Kishapu Sefu Rashidi, amempongeza Rais Samia kwa sadaka hiyo ambayo ameitoa ya chakula kwa watu wenye mahitaji maalumu, na kwamba wanamuombea kwa mwenyezi mungu aendelee kuwa na afya njema ili watumikie watanzania.
TAZAMA PICHA👇👇
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mboni Mhita,ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kahama zawadi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mboni Mhita,ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kahama akionyesha upendo kwa mtoto.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464