MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA MABALA MLOLWA AENDELEA NA ZIARA YA KUWAFUNDA WENYEVITI WA VIJIJINI NA VITONGOJI: ATINGA SHYDC


MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA MABALA MLOLWA AENDELEA NA ZIARA YA KUWAFUNDA WENYEVITI WA VIJIJINI NA VITONGOJI: ATINGA SHYDC
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ndugu Mabala K. Mlolwa ameendelea na ziara ya kuwafunda Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji, Shinyanga vijijini na kukutana na Wenyeviti wa Vijiji 126 na Wenyeviti wa Vitongoji 845. Ziara hiyo iligawanywa katika vituo vinne ambavyo ni Kituo cha Iselamagazi, Solwa, Didia na Samuye ambapo Wenyeviti walijitokeza kwa wingi.

Amefanya ziara hiyo jana.

Pia, Mwenyekiti Mabala, alitumia nafasi hiyo kwanza kuwapongeza Wenyeviti hao kwa kuchaguliwa kisha kuwapa Mafunzo ili wakachape kazi vizuri za kuwatumikia wananchi bila kuwabagua na kuwakumbusha kuwa kama kuna changamoto zozote basi wazitatue kwa kutumia vikao.


Aidha, Mwenyewe Mabala amemshukuru na kumpongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga maana kila Kijiji na vitongoji kimefikiwa na miradi mizuri na ya kimikakati na kutoa tamko 2025 tutasimama na Mama Shinyanga.


Aidha, ndugu Mabala amempongeza pia Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Ally Salum kwa kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi wake hivyo kuwaomba wenyeviti kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Mbunge pamoja na madiwani.


Mwisho, Wenyeviti wamekumbushwa kuisimamia na kuilinda miradi yote iliyotekelezwa katika maeneo yao.


Imetolewa na :-
Ndugu Richard Raphael Masele
Katibu Siasa Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Shinyanga

















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464