RC MACHA ASHIRIKI JUBILEE YA MIAKA 25 YA NDOA YA ASKOFU DKT. NZELU WA KKKT SHINYANGA



RC MACHA ASHIRIKI JUBILEE YA MIAKA 25 YA NDOA YA ASKOFU DKT. NZELU WA KKKT SHINYANGA

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo ameshiriki katika Ibada ya Jubilee ya mika 25 ya ndoa ya Askofu Dkt. Yohana Ernest Nzelu na mke wake Bi. Lilian Gyunda wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, huku akimpongeza kwa kufikia miaka hiyo ya ndoa, na kwamba amemshukuru kwa kuendelea kufanya kazi na Serikali wakati wote, ambapo waumini ambao ni mazao mema kwa Kanisa na anawaongoza yeye ndiyo hao ambao Serikali inawatumikia.

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 21 Desemba, 2024 wakati Ibada hii ambayo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Shinyanga na Simiyu akiwemo Askofu mstaafu Dkt. Emmanuel Makala, ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa Serikali inatambua, kuthamini na kwamba itaendelea kufanya kazi na viongozi wa madhehebu ya dini zote likiwemo kanisa la KKKT ili kuleta amani, maendeleo na mshikamano katika muktadha wa ustawi wa Watanzania na Taifa letu kwa ujumla.
"Nakupongeza sana Baba na Mama Askofu Dkt. Yohana Ernest Nzelu kwa kufikia siku hii ya leo na kuadhimisha Jubilee ya miaka 25 ya ndoa yenu, Mwenyezi Mungu awabariki sana na kwa upande wa Serikali tuseme tu kuwa tunatambua, kuthamini na tutaendelea kufanya kazi zinazofanywa na Madhehebu yote likiwemo hili la KKKT unaloliongoza ili tunaowahudumia wawe na ustawi wa maisha yao kiroho, kimwili, na kulinda amani yetu na ya Taifa kwa ujumla," amesema RC Macha.

KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lilimchagua Askofu Dkt. Yohana Ernest Nzelu, kuwa Askofu wa pili wa Dayosisi hiyo, baada ya kufanya uchaguzi katika mkutano mkuu uliofanyika Desemba 9-10, 2022 katika Usharika wa Tumaini Bariadi mkoani Simiyu na ambaye leo hii anatimiza miaka 25 ya ndoa yake.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464