HELP AGE WAENDESHA MAJADILIANO KWA MAKUNDI RIKA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI KAHAMA
SHIRIKA la Help Age Tanzania,limeendesha majadiliano kwa makundi rika wilayani Kahama kwa ajili ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake,watoto, ndoa za utotoni,na kusaidia kuimarisha ushiriki wa wanaume katika masuala ya Afya ya uzazi na haki.
Majadiliano hayo yamefanyika leo Desemba 13,2024 katika Kata mbili za Manispaa ya Kahama, ambazo ni Nyahanga na Nyandekwa.
Afisa ufuatiliaji kutoka Help Age Winnie Hinaya, amesema Majadiliano hayo ni utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu, ambao unafadhiliwa na serikali ya Finland kupitia Shirika la UNFPA,kwa mgawanyo wa majukumu na kwamba Help Age imekasimishwa eneo la kuendesha kwa wanaume,vijana, na jamii kwa ujumla ili kubadilisha mitazamo,na fikra katika kupunguza ukatili ndani ya jamii na kuimarisha ushirikia wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na haki.
Amesema majadiliano hayo,wameshirikisha makundi rika yote wakiwamo vijana,wanawake,mabinti wazee,watu wenye ulemavu,viongozi wa dini, Polisi Kata, Maofisa Maendeleo na Ustawi wa jamii, ili wajadili ukatili uliopo na namna ya kuchukua hatua kuudhibiti.
"Mradi huu wa chaguo langu haki yangu,watekelezaji wakubwa ni Help Age ambapo hapa Kahama tunautekeleza katika Kata ya Nyahanga, Nyandekwa, Kagongwa,Mongolo,Mungula,Nyasubi na Majengo,"amesema Winnie.
Washirikia wakizungumza katika majadiliano hayo kwa nyakati tofauti,wamesema bado jamii inaukatili wa kiuchumi kwa kunyanyasa wanawake, kutelekeza watoto,vipigo kwa wanawake, wanaume kunyimwa haki zao na wake zao,watu wenye ulemavu kunyimwa haki zao.
Ukatili mwingine walioutaja ni wazee kudhauriwa na watoto,sababu ya kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili, pamoja na kuendelea kwa ndoa za utotoni.
Katibu wa jukwaa la wanawake Kata ya Nyahanga Halima Hussein,ametoa ushuhuda kwenye majadiliano hayo,kwamba jana tu alipokea taarifa juu ya mama mmoja ambaye ni jirani yake, kuwa anasiku tatu amefukuzwa na mumewake,huku akiwa amepigwa vibaya,lakini alizungumza na wana ndoa hao na kusuhuhisha,sababu makosa yalikuwa ya kusameheana.
Mwenyekiti wa Baraza la usuluhishi Kata ya Nyahanga Geogre Simba, amesema wamekuwa wakipokea kesi nyingi za wanawake kudai taraka, kutokana na migogoro ya kiuchumi.
Polisi Kata wa Nyahanga Annanias Kashaija, amesema migogoro mingi ya ndoa inatokana na watu kuishi kimazoea, pamoja na kuendekeza mifumo dume.
Naye mzee Elizabeth Rubasha kutoka Nyandekwa, ukatili wa kijinsia kwa sasa umekuwa na utandawazi kwa kuiga mambo ya kigeni.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashuri ya Manispaa ya Kahama Ester Mkumbae, amesema ukatili wa kijisia bado upo kwa jamii japo siyo kwa kiwango kikubwa,kutoka na kuendelea kutoa elimu wakishirikiana na mashirika.
Amesema vitendo vya ukatili ambavyo vimetajwa na wananchi wa Kata hizo mbili Nyahanga na Nyandekwa,bado vipo na kwamba Serikali hua wanachukua hatua.
TAZAMA PICHA👇👇
Afisa ufuatiliaji kutoka Help Age Winnie Hinaya,akizungumza kwenye mjadiliano hayo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashuri ya Manispaa ya Kahama Ester Mkumbae,akizungumza kwenye majadiliano hayo.
Washiriki wakiendelea na majadiliano.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464