HOFU,IMANI ZA KISHIRIKINA NA UCHAWI VIKWAZO UTOAJI TAARIFA NA USHAHIDI MATUKIO YA UKATILI KISHAPU
Na SUMAI SALUM-KISHAPU
Shirika lisilokuwa la kiserikali la kusaidia wazee lenye makao yake makuu jijini Dar es salam linalotekeleza mradi wa Chaguo langu haki yangu katika kata Saba za halamashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga limewakutanisha wadau kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa mradi huo huku elimu ya utoaji taarifa na ushahidi ikionekana kuwa tatizo kwa jamii hizo.
Kikao kazi hicho cha tathimini kilichofanyika December 18,2024 katika ukumbi wa chuo cha ufundi stadi VETA Wilayani humo kimejumuisha wanufaika ambao ni wanamabadiliko ngazi ya jamii kutoka kata za mradi ikiwemo Lagana,Talaga,Ukenyenge,Mwaweja,Mwamalasa,Idukilo pamoja na Mwamashele.
Akiwasilisha taarifa ya mradi katika kata ya Mwamashele Mtendaji wa kata Lilian Sixbert amesema mradi huo ameongeza ujasiri na utoaji taarifa katika kata hiyo ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
"Katika kijiji cha Bubinza kuliripotiwa taarifa za kuolewa kwa binti mmoja chini ya miaka 18 tukalizuia hilo ila baba mzazi aliweka chuki na baadhi ya majirani akidhania ndio wametoa taarifa tukajitahidi kuwaweka sawa na taratibu zingine za kisheria zinaendelea" amesema Lilian.
Katika kata ya Lagana akisoma taarifa mtendaji wa kata hiyo Kashinje Ikombe amesema mradi huo umekuwa chachu ya mabadiliko kwa wanaume kutoa taarifa za ukatili mbalimbali wanaokutana nao ikiwa ni pamoja na ukatili wa kiuchumi inayopelekea baadhi ya wanaume kunyimwa tendo la ndoa na ofisi yake imekuwa ikiwakumbusha falsafa ya ndoa na ndoa zinakuwa salama.
Sambamba na hayo wakitoa maoni juu ya sababu ya kutotoa taarifa za ukatili wa kijinsia na ushahidi Mzee.Godfrey Nkonji wa Ukenyenge ametaja sababu ya imani ya kishirikina na uchawi kuwa ni sababu ambayo wengi wanaogopa hivyo jamii inahitajika ijengewe uwezo wa kujiamini.
Kwa upande wake Clara Andrew amesema watu wengi wanashindwa kutoa taarifa na ushahidi kwenye taarifa za ukatili wa kijinsia kutokana na ucheleweshwaji wa utoaji hukumu pamoja na kuwepo kwa migogoro baina ya familia na familia na kupelekea uadui wa kudumu.
Nae mwenyekiti wa kitongoji cha Mwamagili kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge John Lugembe Sheka amesema mradi wa Chaguo langu haki yangu umemnufahisha kwa kujengewa ujasiri wa kujiamini licha ya kuwa na ulemavu wa miguu katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita aligombea nafasi ya mwenyekiti wa kijiji licha ya kuwa hajapata amekuwa mwenyekiti wa kitongoji hicho.
Hivyo wadau hao wamejadili kwa makundi hatua mbalimbali zitakazotumika ili kuisaidia jamii kuwa na utayari wa kutoa taarifa na ushahidi juu ya matukio wamependekeza mambo mbalimbali ikiwemo Utoaji elimu ya kupinga ukatili na kuondoa uoga,uanzishaji clubs mashuleni,polisi kujenga mahusiano mazuri na wananchi,kuondoa mila na desturi kandamizi,kuimarisha elimu ya malezi kwa wazazi na walezi na kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa kwa ngazi zote.
Ikumbukwe mradi wa Chaguo langu haki yangu unaotekelezwa na Helpage ukifadhiriwa na serkali ya Finland na kuratibiwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na idadi ya watu na masuala ya afya ya uzazi na haki UNFPA umejikita katika mapambano dhidi ya ukatili,unyanyasaji na utekelezaji katika eneo la mabadiliko ya tabia kwa kuwajengea uwezo wavulana na wanaume ili wawe na mtizamo chanya pamoja na kuendesha majadiliano ya makundirika.0
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464