VYAMA VITANO VYA UPINZANI SHINYANGA VYAPONGEZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VYALIA NA DOSARI NDOGO NGOGO

 

VYAMA VITANO VYA UPINZANI SHINYANGA VYAPONGEZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VYALIA NA DOSARI NDOGO NGOGO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

VYAMA vya upinzani mkoani Shinyanga,baadhi vimeridhika na uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika novemba 27 mwaka huu,huku zikiomba dosari ndogo ndogo ambazo zilijitokeza, kwamba zisijitokeze kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Rehema Bulilo Katibu wa Chama cha SAU mkoani Shinyanga.

Vyama hivyo ni CUF, Demokrasia Makini,NRA,CHAUMA pamoja na SAU.

Viongozi wa vyama hivyo wamebainisha hayo leo Desemba 2,2024 wakati wakizungumza na vyombo vya habari kutoa tathimini ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika novemba 27,2024.
Johari Mlyomi Katibu wa CHAUMA Mkoa wa Shinyanga.

Wamesema uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa umefanyika vizuri kwa Amani na hapakutokea vurugu zozote, isipokuwa uligubikwa na dosari ndogo ndogo,ikiwamo baadhi ya watu ambao siyo waaminifu kuiba kura,pamoja na kukosekana majina kwenye baadhi ya vituo vya kupigia kura,na kuomba uchaguzi mkuu 2025 zisijitokeze dosari hizo.

Mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma (CHAUMA)Mkoa wa Shinyanga Rashidi Katabanya,amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 umefanyika kwa amani na ulikuwa mzuri, isipokuwa hizo dosari ndogo ndogo, na kuiomba serikali katika uchaguzi mkuu mwakani 2025 ijipange vizuri ili uwe huru na haki.
Grace Mnyasi Katibu wa Chama cha Demokrasia Makini.

Naye Grace Mnyasi Katibu wa Chama cha Demokrasia Makini mkoani Shinyanga, amesema licha ya uchaguzi huo kugubikwa na dosari ndogo ndogo, lakini ulizingatia demokrasia na kuipongeza Tume ya uchaguzi kwa maandalizi mazuri.

Aidha,katika uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa uliofanyika novemba 27,2024, Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliibuka na ushindi kwa kupata viti vingi, tofauti na wapinzani ambao waliambuliwa viti vichache.

TAZAMA PICHA 👇👇
Katibu wa Chama cha NRA Mkoa wa Shinyanga Edward Jisandu akizungumza na waandishi wa habari kutoa tathimini juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27 ,2024
Mwenyekiti wa CHAUMA Mkoa wa Shinyanga Rashidi Katabuya akizungumza na waandishi wa habari kutoa tahimini juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27,2024.
Athumani Salum Katibu wa CUF Mkoa wa Shinyanga akizungumza na waandishi wa habari kutoa tathimini juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika novemba 27,2024.
Rehema Bulilo Katibu wa chama cha SAU mkoani Shinyanga.
Picha ya pamoja.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464