WASHINDI BONANZA LA MICHEZO DR.SAMIA/JUMBE HOLIDAY WAONDOKA NA ZAWADI ZAO,MHANDISI JUMBE AAHIDI KUENDELEZA MICHEZO SHINYANGA


WASHINDI BONANZA LA MICHEZO DR.SAMIA/JUMBE HOLIDAY WAONDOKA NA ZAWADI ZAO,MHANDISI JUMBE AAHIDI KUENDELEZA MICHEZO SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
BONANZA la Michezo Dr.Samia/Jumbe Holiday limefana mjini Shinyanga, huku wakishindi wakiondoka na zawadi zao mbalimbali zikiwamo fedha Taslimu.

Bonanza hilo la kufunga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka mpya 2025, limefanyika katika Viwanja vya CCM Kambarage Mjini Shinyanga, ambapo mchezo wa mwisho mpira wa kikapu unafanyika katika viwanja ya Risasi ili kuupokea mwaka mpya.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe,ambaye ndiye ameandaa bonanza hilo, amesema amefarijika kuona muitiko mkubwa wa wananchi kushiriki michezo mbambalimbali, na kuahidi kuendeleza michezo katika manispaa ya Shinyanga.

“Mji wa shinyanga umepoa sana, sisi kama wazawa wa hapa shinyanga, lazima tushirikiane kuuchangamsha, na kuukuza mji wetu na kuleta burudani mbalimbali, sababu michezo pia ni ajira,ina imarisha afya,kudumisha amani, mshikamano,kuleta umoja na inatoa stress pia,”amesema Mhandisi Jumbe.

“2025 tutafanya mambo makubwa pia ikiwamo na kuleta matamasha ya music, na nitaanza pia na kombe la mpira wa pete na kualika timu kutoka wilaya jirani,”ameongeza.

Nao baadhi ya washiriki wa michezo katika bonanza hilo, wamemshukuru Jumbe kwa kuunga mkono sekta ya michezo, ambayo ni fursa kwa vijana katika kupata ajira.
Aidha, michezo mbalimbali iliyochezwa katika bonanza hilo ni mbio za baiskeli, mchezo wa bao,drafti,karata,Ps Game,Mpira wa pete,kikapu,kufukuza kuku kwa jinsia zote,kushindana kula na Polltable.

Michezo mengine ni mpira wa miguu kati ya bodaboda dhidi bajaji ambapo Bajaji wameibuka washindi, timu ya wilaya ‘Ranges’ dhidi ya Ngokolo, ambapo Ngokolo wameibuka washindi, pamoja na DERBY ya upongoji iliyoisha kwa mikwaju ya penati.
Zawadi zilizotolewa kwa washindi ni fedha,mchele,soda, kuku pamoja na ng’ombe.

TAZAMA PICHA👇👇
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akizungumza kwenye bonanza hilo.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akikabidhi zawadi kwa washindi.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akikabidhi zawadi kwa washindi.
Ng'ombe ambazo ni zawadi za washindi.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akisalimiana na wachezaji.
Michezo ikiendelea.
Mashindano ya kula.
Mashindano ya kunywa juice.
Mratibu wa bonanza la michezo Dr.Samia /Jumbe Holiday Jackline Isaro akicheza bao.
Mashindano yakiendelea.
Mbio za baiskeli.
Mshindano ya Polltable.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akiendesha baiskeli.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464