KATAMBI AFANYA MAKUBWA KATIKA SEKTA YA ELIMU,



Na Mwandishi wetu , Shinyangapress blog

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi aeleza mafanikio aliyoyafanya ndani ya miaka minne katika sekta ya Elimu, ambapo amesema mwaka 2020 shule za sekondari na msingi zilikuwa 65 na katika kipindi cha 2020 hadi 2024 zimeongezeka shule tisa na kufikia jumla ya shule 74.

Katambi amesema katika kutekeleza sekta ya Elimu jimbo la Shinyanga mjini kwa kipindi cha miaka minne shule hizo ni pamoja na shule ya sekondari Mwangulumbi, Shule ya sekondari Butengwa, Shule ya Sekondari Lubaga, Shule ya sekondari ya wasichana Shinyanga, Shule ya msingi mwamashele, Shule ya msingi mwamagulya, Shule ya msingi Itongwang'olo, Shule ya msingi Ibadakuli na Shule ya msingi Mwasane.

Katika kuboresha na kuimarisha miundombinu ya Shule Jumla ya Vyumba vya madarasa 176 Vyenye Thamani ya 3,520,000,000 tayari vimejengwa na vimekamilika,Ujenzi wa Bweni shule ya msingi Buhangija wenye thamani ya 190,000,000/, ujenzi wa Mabweni manne (4) Shule ya sekondari Old shinyanga yenye thamani ya 544,000,000.

Ukarabati wa Chuo cha maendeleo ya wananchi(FDC) Buhangija wenye gharama ya 650,000,000.

Katambi amewaomba wananchi wa jimbo la Shinyanga waendelee kumuamini ili aendelee kufanya mambo makubwa zaidi katika sekta ya elimu.

Pia amefanya maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo miundombinu ya barabara, maji,umeme na afya 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464