VIONGOZI WA DINI WAGANGA WA KIENYEJI NA SUNGUSUNGU WAPEWE ELIMU YA KUHAMASISHA MASUALA YA LISHE ILI KUONDOA UTAPIA MLO KWA WATOTO


Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga


Na Suzy Butondo, Shinyangapress blog

Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Shinyanga wametoa ushauri kwa serikali kwamba viongozi wa dini Waganga wa kienyeji na Sungusungu wapewa elimu ya kuhamasha masuala ya lishe kwenye jamii ili kuondoa utapia mlo kwa watoto walio chini ya miaka mitano, kwani hadi sasa utapia mlo umefikia asilimia 27.5 ambapo mwaka 2022 ilikuwa asilimia 31.1.

Hayo yamesemwa hivi karibuni kwenye semina ya siku mbili ya lishe yenye malengo ya kuboresha sera, na mazingira ambayo yataleta uboleshaji wa huduma kwa watoto, wanawake na wanaume, iliyofanyika mkoani Shinyanga nakuandaliwa na shirika la Word Visioni na Kivulini.

Wakichangia hoja mbalimbali kwenye semina hiyo wawakilishi wa mashirika mbalimbali mkoani Shinyanga akiwemo Piter Shimba kutoka taasisi ya Msalala amesema ili kuongeza wigo wa uhamasishaji ni vizuri waganga wa kienyeji, viongozi wa dini na sungu sungu wakahamasisha jamii ili izingatie masuala ya lishe bora.

"Waganga wakienyeji wanaaminika sana kwenye jamii wakisema jambo wananchi wanaelewa hivyo ni vizuri wakapatiwa elimu ya kuhamasisha ili tuweze kusaidizana nao pamoja na viongozi wa dini, kwani wanakuwa na waumini wengi ambao wanawafundisha neno la Mungu, hivyo ni rahisi kuhamasisha suala la lishe ili kupunguza utapia mlo kwa watoto",amesema Shimba.

Afisa lishe kutoka wilaya ya Kishapu Hadija Ahmed akiwasilisha taarifa ya mkoa amesema hali ya utapiamlo katika mkoa wa Shinyanga imefikia asilimia 27.5 kutokana na changamoto ya utapia mlo wanahamasisha kaya kama haina chakula wauze mifugo ili watoto wapate lishe na kutouza mazao ya chakula kiholela wakati wa mavuno.

"Changamoto ya kwanza ushiriki mdogo kwa wanaume na mira na desturi ambayo ni mfumo wa maisha, kwani tiba asili kwa watu wa Shinyanga wakiugua wanaanzia kwa waganga kwanza hawaanzii hospitali hali ambayo imekuwa ikisababisha udumavu na kusababisha vifo vingi vya watoto walio chini ya miaka mitano, hivyo wamekuwa wakiwapeleka hosipitali wakiwa wamechoka kutoka kwa waganga wa kienyeji",amesema Hadija.

"Kupungua kwa utapiamlo mkali kwa watoto chini ya miakamitano kutokaasilimia 32.1 kwa mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 27.5, mwaka 2022 Uzito pungufu 13.3 hadi 8.6 na ukondefu 4.3 hadi 1.3" ambapo jukumu la kupambana na utapia mlo niombe liwe kipaumbele kwa kila mshiriki ili kwa pamoja tuweze kupunguza madhara yatokanayo na lishe duni katika jamii",ameeleza Hadija.

Pia amesema wazazi ni vizuri wakachangia chakula mashuleni, ili watoto waweze kufaulu vizuri, kwani mtoto asipopata chakula bora hata ufaulu wake unakuwa chini,hivyo ni vizuri kuwahamasisha wazazi waendelee kuchangia chakula mashuleni, kwani wasipofanya hivyo ni moja ya kuwanyanyasa watoto kwani wanakuwa njaa kuanzia asubuhi hadi jioni.

Meneja mradi Grow Enrich wa World Vision Tanzania Shukrani Dickson alisema kuna mkakati madhubuti wa kuifikia jamii na kuihamasisha kuwaandalia watoto milo kamili, hivyo ni vizuri wadau wote wa lishe kwenda kuongeza nguvu ya pamoja kwa kushirikiana na serikali katika kuweka kipaumbele vya lishe.

"Idadi kubwa ya wanawake wamekuwa hawanyonyeshi watoto na kuwaaandalia chakula cha lishe kuyokana na ubize wq shughuli walizonazo, hivyo twendeni tukahamasishe wazazi wanyonyeshe watoto kwa wakati ili kuondokana na udumavu, pia tuwashirikishe mama wakwe zao ili wawanyonyeshe, hii yote ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu ili kuhakikisha malengo ya serikali yetu yanatimia",amesema Shukrani.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Shirika la Kivulini lenye makao makuu yake Mwanza Yasin Ally alisema kazi kubwa iliyopo ni kutekeleza mikakati iliyopo kwa ajili ya kuimalisha masuala ya lishe na kuwezesha maazimio ya nchi yaliyowekwa 2021 ya kupunguza kiwango cha asilimia 10 na kuhakikisha changamoto ya utapia mlo, ukatili.

 
"Moja ya shughuli zetu ni kushughulikia. ukatili wa kijinsia, lishe ya mtoto, afya ya mama na mtoto, wanaume, viongozi wa dini ili kuhakikisha ni namna gani tutafikisha mabadiliko ngazi ya kaya, tunawekeza kwa mabadiliko ya mtu mmoja mmoja tunashirikisha wanaume wanawake ili kuona wanamsapotije mama mjamzito", amesema Ally.

"Pia tunawekeza kutoa elimu ya madhara ya ukatili wa kijinsia wa kiuchumi, ili kuona mavuno yanatumikaje ngazi ya familia, tunatoa elimu kwa kushirikisha kaya na mikutano ya hadhara, kwenye maadhimisho tunahakikisha, tushirikisha vikundi mbalimbali ili kuhakikisha changamoto za ukatili wa kijinsia zinatoweka katika jamii",aliongeza.

"Aidha mashuleni tunakuwa na midahalo ambayo inahusisha wanafunzi na walimu kwani changamoto iliyopo watoto wengi wanalazimisha kupanga karibu na shule ambapo wazazi wanawapa debe la unga tu na dagaa, hali ambayo watoto wengi wanakuwa wadumavu, pia ulinzi na usalama haupo kwani wanaweza kufanyiwa ukatili bila kujua mzazi wakiwa katika nyumba hizo za kupanga"

Amesema kutokana na ukatili huo wanahakikisha kaya nyingi zinaelimishwa na kuondokana na ukatili wa kutowatekelezea watoto wao lishe bora, kwani wamekuwa wakilima wanawake hawafaidiki na mavuno yao na wanaendelea kulalia godolo la nyasi, fedha za mavuno wanazovuna wanaume wanapeleka kuhonga wanawake wengine, hivyo tumehamasisha wameendelea kuhamasisha na baadhi ya kaya zinaelewa.

Naye afisa lishe kutoka wizara ya afya Bagelela Magana amesema, mikakati ya sekta ya afya kwa kushirikiana na sekta ya elimu katika kukabiliana na udumavu kwa watoto ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa programu ya lishe, lengo likiwani ni kupunguza utapia mlo wa virutubisho pamoja na madini.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga

Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMeneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
 
Afisa Lishe kutoka Wizara ya Afya, Bagelela Kagiye Magana akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Afisa Lishe kutoka Wizara ya Afya, Bagelela Kagiye Magana akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mtalaam wa Afya na Lishe kutoka World Vision Tanzania, Elizabeth Ndaba akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mtalaam wa Afya na Lishe kutoka World Vision Tanzania, Elizabeth Ndaba akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mtalaam wa Afya na Lishe kutoka World Vision Tanzania, Elizabeth Ndaba akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Afisa Lishe Manispaa ya Shinyanga Bestina Gunje akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi kutoka TAMISEMI, Riziki Mbilinyi akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMwakilishi kutoka TAMISEMI, Riziki Mbilinyi akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Afisa Lishe kutoka Wilaya ya Kishapu, Hadija Ahmed Nchakwi akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Wadau wakipiga picha ya pamoja wakati wa warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464