MRADI WA PEPFAR/CDC AFYA HATUA WATOA PIKIPIKI 40 KUIMARISHA HUDUMA ZA VVU KATIKA MKOA WA KIGOMA

Muonekano wa sehemu ya pikipiki 40 zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Mkurugenzi wa Tiba na Matunzo wa THPS, Dkt. Frederick Ndossi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye pikipiki 40 zenye thamani ya shilingi Milioni 141. 4 .

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), linalotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC), limetoa pikipiki 40 zenye thamani ya  shilingi 141,400,000/= sawa na USD 52,370.40 kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma. 

Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye, na Mkurugenzi wa Tiba na Matunzo wa THPS, Dkt. Frederick Ndossi, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia katika hafla iliyofanyika Desemba 13, 2024, katika Viwanja vya Ofisi ya NSSF, Manispaa ya Kigoma.

Dkt. Ndossi ameeleza kuwa pikipiki hizo zitasaidia katika kufikisha huduma za VVU kwa watu wanaoishi mbali na vituo vya afya lakini pia Pikipiki hizi zitawasaidia watoa huduma kufika kwa wananchi kwa ajili ya upimaji wa VVU, utoaji wa dawa za ARV, huduma za kinga dhidi ya VVU (PrEP), na uhamasishaji wa matumizi ya kondomu. 

Vilevile, zitasaidia katika kusafirisha sampuli za makohozi kwa uchunguzi wa Kifua Kikuu na sampuli za damu kwa ajili ya vipimo vya wingi wa virusi vya UKIMWI (HVL).

Dkt. Ndossi amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha matumizi bora ya pikipiki hizi kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kigoma, na kwamba makubaliano ya matumizi ya pikipiki hizi yameainishwa katika mkataba rasmi (MOU).
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 40. 

Pamoja na hayo, Dkt. Ndossi ameeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana mkoani Kigoma tangu mwaka 2011 walipoanza kutoa huduma za VVU/UKIMWI, ikiwa ni pamoja na kuongeza vituo vya kutoa huduma hadi kufikia 74, na kuhakikisha watu wengi wanaoishi na VVU wanapata matibabu bora na wanaishi maisha ya kawaida. 

Aidha, asilimia 95%-99% ya watoto wanaozaliwa na mama wenye maambukizi ya VVU wanazaliwa bila maambukizi, na wale wanaozaliwa na maambukizi wanapata huduma bora na wanaishi kwa afya njema.

Amesema THPS inaendelea kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Kigoma katika kupambana na VVU na kuhakikisha kuwa lengo la Serikali la kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030 linafikiwa.

Katika hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye, ametoa shukrani kwa PEPFAR, CDC, na THPS kwa msaada wao katika kuboresha huduma za afya. 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye.

Mhe. Andengenye amesisitiza kuwa pikipiki hizi zitasaidia kufikia jamii ambazo bado hazijafikiwa na huduma za afya bora, na kuimarisha mfumo wa afya wa Kigoma. 

Amesema serikali imejitolea kutoa fedha nyingi kuboresha huduma za afya, na pikipiki hizi zitakuwa muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Damas Kayera, ametolea mfano mafanikio ya mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU, ambapo kiwango cha maambukizi kimepungua kutoka asilimia 3.4% mwaka 2012 hadi asilimia 1.7% mwaka 2023.

 Ameishukuru THPS kwa ushirikiano wake na kusema kuwa hii ni mara ya pili pikipiki zinatolewa kwa wilaya za Mkoa wa Kigoma, baada ya kutoa pikipiki 58 awali.

Watoa huduma walionufaika na pikipiki hizo wameeleza kuwa msaada huu utawawezesha kufikia watu wengi zaidi, kuharakisha utoaji wa huduma na kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye akizungumza leo Desemba 13,2024 wakati THPS inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC ikikabidhi pikipiki 40 zenye thamani ya shilingi Milioni 141. 4 kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye akizungumza wakati THPS inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC ikikabidhi pikipiki 40 zenye thamani ya shilingi Milioni 141. 4 kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Mkurugenzi wa Tiba na Matunzo wa THPS, Dkt. Frederick Ndossi, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki 40 zenye thamani ya shilingi Milioni 141. 4  zilizotolewa na THPS kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Damas Kayera akizungumza wakati THPS inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC ikikabidhi pikipiki 40 zenye thamani ya shilingi Milioni 141. 4 kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Mkurugenzi wa Tiba na Matunzo wa THPS, Dkt. Frederick Ndossi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye pikipiki 40 zenye thamani ya shilingi Milioni 141. 4  zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye akiwasha moja kati ya pikipiki 40 zenye thamani ya shilingi Milioni 141. 4  zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye akiwa amepanda katika moja kati ya pikipiki 40 zenye thamani ya shilingi Milioni 141. 4  zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye (katikati) akimkabidhi pikipiki mmoja wa watoa huduma za afya
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye (katikati) akimkabidhi pikipiki mmoja wa watoa huduma za afya
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Mhe. Thobias Andengenye (katikati) akimkabidhi pikipiki mmoja wa watoa huduma za afya
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 40 zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 40 zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 40 zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 40 zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC kwa ajili ya kuboresha huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU katika Mkoa wa Kigoma.
Wadau wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya pikipiki 40 zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC

Picha za kumbukumbu wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki 40 zilizotolewa na THPS  inayotekeleza Mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464