MWENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA AWASHUKURU WANANCHI SHINYANGA MJINI, AWATAKA WAENDELEE KUIAMINI CCM


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mabala Mlolwa akiwashukuru wananchi wa wilaya ya Shinyanga mjini

Suzy Butondo, shinyangapress blog

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amewashukuru wananchi wa wilaya ya Shinyanga mjini kwa kuchagua wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kishindo kikubwa cha asilimia 100.

Shukrani hizo amezitoa leo kwenye mkutano wa hadhara ambao aliufanya kwa lengo la kuwashukru wananchi wa wilaya ya Shinyanga kwa kukichagua chama hicho kwa asimia 100.

Mabala amesema vyama vya upinzani sio adui wa CCM bali ni ndugu wa CCM, kwani wasingekuwepo usingekuwepo ushindi, lakini walishindana na CCM imeibuka kidedea kwa kushinda kwa vijiji vingi na mitaa migi ya kutosha.

"Kwa kweli hawa si adui zetu tunawapenda kwa sababu ni ndugu zetu, kwani wasingekuwepo tungepataje sass ushindi wa kishindo namna hii, tunaomba waendelee kuwepo tu ili tuendelee kudumisha Demokrasia"amesema Mlolwa.

"Rais wetu Samia Suluhu Hassan amepanua Demokrasia na wasingekuwepo tusingejua kama tunakubarika lakini kwa sasa tumejua kwamba tunakubarika kwa wananchi, lakini pia kama anayetaka kuingia CCM karibuni sana, sisi hatuna choyo yoyote ni wakarimu kabisaa pia namshukuru kwa kuleta mabilioni ya fedha kwa ajili ya maendeleo hivyo muendelee kutuamini ili tufanye makubwa zaidi na tumalizie pale ambapo hakujamalizika"amesema mwenyekiti Mlolwa.

Pia Mlolwa amewaomba wenyeviti wasiende kufanya kazi kwa kuwabagua wawatumikia wananchi wote bilakuangalia rangi kabila, hata kama alikuwa mgombea mwenza wawahudumie ipasavyo.


"Nawashukuru sana wananchi katika awamu hii mmeshirikiana vizuri mmetengeneza umoja vizuri na viongozi wa CCM, nawashukuru sana wananchi wa Shinyanga kwa kazi nzuri mliyoifanya niwaombe muwape ushirikiano wenyeviti
wenu mliowachagua ili kuweza kusimamia maendeleo ya kata zetu na wilaya kwa ujumla na Mungu atawabariki"amesema Mabala

Kwa upande wake katibu wa itikadi uenezi na mafunzo Richard Rafael Masele lengo kubwala mkutano huo ni kuwashukuru wananchi wa wilaya ya Shinyanga kwa kuchagua viongozi wa CCM kwa asilimia 100 na kupata mitaa 90 na na vijiji 504.kwa mkoa wa Shinyanga, huku manispaa ikichukua  mitaa 55 vijiji 17 vitongoji 82 Chadema kitongoji kimoja 

"Na ushindi huu ni mvua za rasha rasha uchaguzi wa mvua kubwa utakuwa mwakani ndiyo mvua itawanyeshea,tunamshukuru Rais Samia Suluhu kwa maendeleo kwani kila mahali pamefikiwa, zahanati, vituo vya afya, maji, Elimu, na miundombinu ya barabara,"amesema Masele.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mabala Mlolwa akiwashukuru wananchi wa wilaya ya Shinyanga mjini
Katibu wa itikadi na uenezi na mafunzo Richard Rafael Masele akizungumza na wananchi wa wilaya ya Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Anold Makombe akizungumza na wananchi wa Shinyanga mjini
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Naibu Katalambula akizungumza



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464