Polisi shinyanga wakamata silaha Gobore ikiwa imepakiwa kwenye baiskeli
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limekamata silaha aina ya Gobore katika kijiji cha Bugomba A Kata ya Ulewe Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, ikiwa imepakiwa kwenye baiskeli,huku mtuhumiwa akikimbia mara baada ya kuona gari la polisi.
Hayo yamebaimishwa leo na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, kufuatia msako ambao wameufanya kuanzia novemba 27 hadi Desemba 22,2024.
Amesema katika msako huo, wamekata jumla ya watu 81 na vielelezo mbalimbali, ikiwamo silaha aina ya Gobore
madini bandia gramu 250 yadhaniwayo kuwa ni dhahabu.
Vielelezo vingine ni bangi gramu 9,000,mirungi bunda tisa, Gongo lita 113,Sola panel Saba,betri Nne za Sola,pikipiki 11,kadi tatu za pikipiki,Antena Nne za Ving'amuzi.
Vingine ni redio mbili,baiskeli mbili,mashine moja ya bonanza,kamera moja, na mitambo minne ya kutengeneza Gongo.
Aidha,amesema kwa upande wa makosa ya usalama barabarani,wamekamata makosa 5,376, Magari 3,767, Bajaji na Pikipiki 1609, na wahusika waliwajibishwa na kulipa faini za papo kwa papo.
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu,huku akiwakumbusha wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.