TRA SHINYANGA YAWASHUKURU WALIPA KODI KWA KULIPA KODI KWA HIARI

Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akizungumza wakati Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa wa TRA walipotembelea kampuni hiyo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, amewashukuru na kuwapongeza wafanyabiashara wa makampuni ya GAKI Transporters Ltd na Gilitu Enterprises Ltd kwa kujitolea kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati. 

Pongezi hizo amezitoa katika ziara aliyoifanya leo, Jumatatu Desemba 16, 2024, akiwa na maafisa wengine wa TRA, ambapo wamekutana na wamiliki wa makampuni hayo na kusikiliza changamoto zao.

Maro amesema kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa mfano mzuri wa walipa kodi ambao wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari na kwa usahihi, jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa taifa. 

Amesisitiza kuwa, TRA itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwa ufanisi zaidi.

Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (katikati), na maafisa wengine wa TRA  wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo 

"Nyinyi ni walipa kodi wazuri na mna mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa letu. Tumekuja kuwashukuru kwa kulipa kodi kwa hiari, lakini pia ili kusikiliza changamoto zenu na kupokea maoni. Ushirikiano wenu na TRA ni muhimu, na tunawatia moyo muendelee na mfano huu," amesema Maro.

Maro pia amewahimiza wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za manunuzi na matumizi ya mashine za EFDs (Electronic Fiscal Devices) ili kuboresha uwazi na ufanisi katika ulipaji wa kodi. 

Amesema kuwa matumizi ya EFDs ni muhimu kwa kuhakikisha kila muamala unarekodiwa na kodi inalipwa ipasavyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo, ameeleza kuridhika na huduma inayotolewa na TRA, akitaja kuwa, kwa sasa, wafanyabiashara wengi wanapata huduma bora na elimu kuhusu masuala ya kodi. 

 Gaspar Kileo (GAKI)

Kileo amesema kuwa, tofauti na zamani ambapo wafanyabiashara walikuwa wakishurutishwa kulipa kodi, sasa wanatoa kodi kwa hiari na kwa furaha kutokana na uhusiano mzuri na maafisa wa TRA.

"TRA ya sasa inafanya kazi nzuri. Huduma kwa wateja ni bora na tumekuwa tukifundishwa masuala ya kodi. Sasa hivi tunalipa kodi kwa hiari, tofauti na ilivyokuwa zamani," amesema Kileo.

Mkurugenzi wa Gilitu Enterprises Ltd, Gilitu Makula, amesisitiza umuhimu wa kulipa kodi kama sehemu ya maendeleo ya biashara na taifa kwa ujumla. 

Makula ameeleza kuwa anajivunia kuwa mwekezaji mzawa anayeunga mkono juhudi za serikali katika kukusanya mapato.

 Gilitu Makula 

 Ameongeza kuwa, kwa sasa wafanyabiashara wengi wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kwa usahihi na kutunza kumbukumbu za malipo.

"Mimi kama Mtanzania, najivunia kulipa kodi kwa wakati. Bila kodi hatuwezi kuendelea kama nchi. Ni muhimu tuendelee kuelimishana kuhusu umuhimu wa kodi na kuhakikisha tunalipa kwa usahihi," amesema Makula.

Ziara hiyo imekuwa ni sehemu ya juhudi za TRA kukuza ushirikiano na walipa kodi, na kutoa elimu zaidi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari na kwa usahihi. 

Wafanyabiashara wa Shinyanga wameonyesha mfano mzuri wa ushirikiano na TRA, na kuonyesha umuhimu wa kulipa kodi kama njia ya kuimarisha uchumi wa taifa.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (kushoto) akizungumza alipotembelea Kampuni ya GAKI Transporters Ltd (GAKI Investment na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited (EASTL) leo Jumatatu Desemba 16,2024. Katikati ni Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (katikati) akizungumza alipotembelea Kampuni ya GAKI Transporters Ltd (GAKI Investment na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited (EASTL) 
Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo akizungumza wakati Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, na maafisa wengine wa TRA akiwemo Meneja Msaidizi Huduma ya Mlipa Kodi Ramadhan Sengo walipotembelea kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo akizungumza na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (kushoto).
Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo akimuongoza Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, na maafisa wengine wa TRA kuangalia namna wanavyozalisha Vinywaji Vikali (Goldberg , Hanson's Lite, Diamond Rock na Hanson's Choice) katika kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL)
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, na maafisa wengine wa TRA wakiangalia namna uzalishalishaji wa Vinywaji Vikali (Goldberg , Hanson's Lite, Diamond Rock na Hanson's Choice) unavyofanyika katika kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL)

Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (mwenye suti ya bluu) , na maafisa wengine wa TRA wakiangalia namna uzalishalishaji wa Vinywaji Vikali (Goldberg , Hanson's Lite, Diamond Rock na Hanson's Choice) unavyofanyika katika kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL)
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro akipiga picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo (kushoto)
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula  alipotembelea Kampuni hiyo 
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro akizungumza alipotembelea Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (wa pili kushoto) akizungumza alipotembelea Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akizungumza wakati Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa wa TRA walipotembelea kampuni hiyo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akizungumza wakati Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa wa TRA walipotembelea kampuni hiyo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akizungumza wakati Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa wa TRA walipotembelea kampuni hiyo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akizungumza wakati Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa wa TRA walipotembelea kampuni hiyo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula (kushoto) akipiga picha ya kumbukumbu na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa wa TRA walipotembelea kampuni hiyo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akielezea namna wanavyozalisha mafuta ya alizeti
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akiwatembeza maafisa wa TRA katika kiwanda cha uzalishaji mafuta
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akielezea namna wanavyozalisha mafuta ya alizeti
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa kutoka TRA wakiendelea kupata maelezo namna uzalishaji wa mafuta unavyofanyika
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa kutoka TRA  wakiondoka katika Mtambo wa Solvent unaokamua mafuta ya pamba katika kiwanda chake cha mafuta ya pamba na alizeti 'SANICO' kilichopo Mjini Shinyanga

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464