![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgArhrIv-1oB3CQo_9ssOpwQzG6ldZmtYSDnB8RfiP39a_m8K9NUqqceCveZvPRwXj0N-Fbpb8EFUoIJdTXuuIMV6nperZP_fcgt3RiXNQsWguefOypqkd5wR-fG93aRn85eQNR6ISDECbv-DjAvI8gRAReCHfL_AsUgx9Uvrc2_gpT-6x7G5z1gsPQEg/s600/2B9A4889.jpg)
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, amemuapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, akimpa majukumu muhimu ya kusimamia amani na kilimo cha pamba, zao kuu la biashara la wilaya hiyo.
Hafla ya uapisho, iliyofanyika leo Januari 27,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na vyama vya siasa.
Akizungumza baada ya kumwapisha, Mhe. Macha amesisitiza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Masindi kwa kuzingatia uwezo wake na mchango wake kwa taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
RC Macha amekazia umuhimu wa kusimamia amani katika wilaya ya Kishapu, akisema: “Rais Samia katika uongozi wake ni kocha, na sisi ni wachezaji. Hivyo, unapaswa kuchapa kazi kwa bidii, kuwatumikia wananchi, na kuhakikisha amani inatawala.”
Ameongeza kuwa kilimo cha pamba ni muhimu kwa uchumi wa wilaya na hivyo Masindi atapaswa kushirikiana na wananchi kutatua changamoto zinazohusiana na zao hilo.
Pia, Macha ameagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha wanafunzi wa darasa la awali, la kwanza, na kidato cha kwanza wanajiandikisha na kuripoti shuleni kwa wakati.
Amewashauri wazazi kuhakikisha watoto wao, wakiwemo wenye ulemavu, wanapelekwa shule bila ubaguzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, amezungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya mkoani humo, akiahidi ushirikiano kwa Masindi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anold Makombe, amesisitiza kuwa Masindi atafanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wenzake ili kutatua changamoto za wananchi.
Akizungumza baada ya kuapishwa, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masindi, amemshukuru Rais Samia kwa kumteua na akasema kwamba atafanya kazi kwa bidii na kuwatumikia wananchi.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgArhrIv-1oB3CQo_9ssOpwQzG6ldZmtYSDnB8RfiP39a_m8K9NUqqceCveZvPRwXj0N-Fbpb8EFUoIJdTXuuIMV6nperZP_fcgt3RiXNQsWguefOypqkd5wR-fG93aRn85eQNR6ISDECbv-DjAvI8gRAReCHfL_AsUgx9Uvrc2_gpT-6x7G5z1gsPQEg/s600/2B9A4889.jpg)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia), akimuapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.
Amesisitiza kuwa anahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi na viongozi wenzake ili kuhakikisha utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Anamringi Macha.
Masindi pia ameeleza kuwa uteuzi wake ulimkuta akiwa shambani akifanya kazi za kilimo, jambo ambalo linampa mtazamo wa kipekee kuhusu umuhimu wa sekta ya kilimo katika maendeleo ya wilaya hiyo.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude, ambaye amehamishwa kwenda Jijini Arusha, ametoa shukrani kwa viongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano waliompa wakati wa utumishi wake na amemtakia Masindi mafanikio katika jukumu lake jipya.
Tarehe 24 Januari 2025, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kuwahamisha wengine kwenye vituo vya kazi, ambapo Peter Masindi, aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nkalama, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu. Uteuzi wake ulimkuta akiwa shambani akendelea na shughuli zake za kilimo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia), akimuapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Jumatatu Januari 27,2025 - Picha na Marco Maduhu na Kadama Malunde
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhANV3T2Qov2VwaxdLQPph1L7a_OSxpkiR_LlUDLpdXDYjUnyLzTv-aTTckytVXLSDFOSf9tTzqRTJOMnq_J8paD-Qvhm8smdZzDVhm5cFuouvSHVy8XqtXXykE5kvAoCJGdH2JS02YwywnXZRasodNkG_MTolVONgatDeYDh7ob1flvM44KBSukQl_w/s600/IMG_7700.jpg)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia), akimuapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Jumatatu Januari 27,2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia), akimuapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Jumatatu Januari 27,2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, akimuapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Jumatatu Januari 27,2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia), akimkabidhi vitendea kazi Peter Masindi baada ya kumwapisha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, akimuapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Jumatatu Januari 27,2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, akimuapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Jumatatu Januari 27,2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia), akimpongeza Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza baada ya kumwapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza baada ya kumwapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu ![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiynxNIclZjixLV3m1aUkL3xIR9jEhCILWKNCIfHD8NnZUfdpyXzkjqDcK87kbkf8Y9HVpoQ4g62vJ6G884EzfxckGktfpK48YNcX7W9ZlU-LVRmdjaSTwY7WoxAJqu9Wa5iHua3o9BtevN0TFAaykzkAPgL5UvjD6iw3FA-QYuWVXhqIzrZ5GjeyhUyw/s600/2B9A5002.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiynxNIclZjixLV3m1aUkL3xIR9jEhCILWKNCIfHD8NnZUfdpyXzkjqDcK87kbkf8Y9HVpoQ4g62vJ6G884EzfxckGktfpK48YNcX7W9ZlU-LVRmdjaSTwY7WoxAJqu9Wa5iHua3o9BtevN0TFAaykzkAPgL5UvjD6iw3FA-QYuWVXhqIzrZ5GjeyhUyw/s600/2B9A5002.jpg)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza baada ya kumwapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza baada ya kumwapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza baada ya kumwapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza baada ya kumwapisha Peter Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mhe. Peter Masindi akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Modest Mkude aliyehamishiwa Wilaya ya Arusha akizungumza na kuwaaga wananchi wa Shinyanga
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Modest Mkude aliyehamishiwa Wilaya ya Arusha akizungumza na kuwaaga wananchi wa Shinyanga
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Modest Mkude aliyehamishiwa Wilaya ya Arusha akizungumza na kuwaaga wananchi wa Shinyanga![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjy-R9pX14JZRf_v0ui1ENeloyDz12nNxrVKt_kl2F-otm9uEQpuegH6mnOpW7LTmoucS80OEXOt_pHbDIaKe-bwdNb6AQEChfpL3Z-2RGqzzXlfF0kenxaeziX3qxY5kH5QrYp9u1p3g9tXRnx1Op7LmGv048u-ZLs69qbFbVYl_Bv6iSJsmqMMx1gMg/s600/2B9A5053.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjy-R9pX14JZRf_v0ui1ENeloyDz12nNxrVKt_kl2F-otm9uEQpuegH6mnOpW7LTmoucS80OEXOt_pHbDIaKe-bwdNb6AQEChfpL3Z-2RGqzzXlfF0kenxaeziX3qxY5kH5QrYp9u1p3g9tXRnx1Op7LmGv048u-ZLs69qbFbVYl_Bv6iSJsmqMMx1gMg/s600/2B9A5053.jpg)
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464