SERIKALI IMETOA AMBULANCE4,GARI LA CHANJO NA PIKIPIKI 10 KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

SERIKALI IMETOA AMBULANCE 4,GARI LA CHANJO NA PIKIPIKI 10 KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI, imetoa magari manne ya wagonjwa (Ambulance),gari la chanjo na pikipiki 10,ili kuboresha huduma za afya mkoani Shinyanga.
Vitendea kazi hivyo zimekabidhiwa leo Januari 2,2025 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Anamringi Macha, kwa Waganga wakuu wa halmashauri na kaimu RMO, hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Hamduni akizungumza katika hafla hiyo ameipongeza serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,kwa kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi na kutoa vitendea kazi hivyo.
“Kwaniaba ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEM ninakabidhi magari manne ya wagonjwa ‘Ambulance’, ambayo yanagawiwa katika halmashauri nne ambazo ni Msalala, Ushetu,Kishapu na Shydc, na gari moja la mkoa kwa ajili ya kusambaza chanjo kwenye halmashauri”amesema CP Hamduni.

“Pikipiki hizi 10, moja inapewa Manispaa ya Kahama,na moja Shinyanga, Msalala inapewa pikipiki mbili, Shydc mbili, Kishapu mbili, na Ushetu mbili, na kazi zake ni kusambaza chanjo kwa wananchi, mara baada ya gari hili la chanjo la mkoa kuzifikisha ngazi ya halmashauri,”ameongeza.
Aidha,ametoa wito kwa waganga wakuu wa halmashauri, kwamba vitendea kazi hivyo wavitunze na vitumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa, huku akiwasihi madereva kwamba waviendeshe kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani, na kwamba atakaye haribu kwa makusudi magari hayo serikali itamchukulia hatua.

Akizungumza kwa upande wa pikipiki za kusambaza chanjo, ameonya kwamba zisije kugeuzwa kwa matumizi ya kufanya biashara ya bodaboda,bali zisaidie wananchi kupata huduma ya chanjo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mlyutu, ambaye ni Mratibu wa Miundombinu ya Afya Mkoa wa Shinyanga,ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya mkoani humo,huku akitoa wito kwa wananchi kwamba katika kampeni zao za chanjo ambazo zitakuwa zikifanyika, wajitokeze kwa wingi kupata chanjo ili kuimarisha afya zao na watoto.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Nuru Yunge, amesema gari la wagonjwa ambalo wamepatiwa pamoja na pikipiki mbili, zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.

TAZAMA PICHA👇👇
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi magari na pikipiki kuboresha huduma za Afya.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mlyutu akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni (kushoto)akimkabidhi gari la kusambaza chanjo kwenye halmashauri, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mlyutu.
Gari la kusambaza chanjo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni (kushoto) nyaraka za gari la wagonjwa Ambulance,Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Kishapu Dk.Godfrey Kisusi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni (kushoto) nyaraka za gari la wagonjwa Ambulance, Mganga Mkuu wa Halmashuri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Nuru Yunge.
Makabidhiano ya Ambulance yakiendelea.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni akiendesha gari la kubeba wagonjwa.
Magari ya kubeba wagonjwa Ambulance.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni (wapili kulia)akikabidhi pikipiki kwa kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Kishapu Godfrey Kisusi, wakwanza ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mlyutu.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mlyutu akiwa kwenye pikipiki.
Pikipiki za kusambaza chanjo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464