MISA-TAN NA PACJI YASAINI MAKUBALIANO YA KUWAJENGEA UWEZO WANACHAMA WA MISA-TAN


Na. Mwandishi wetu

Dodoma

Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tan) imesaini makubaliano na Taasisi ya Pan Africanism Constructive Journalism (PACJI) ili kuwajengea uwezo wanachama wa MISA-TAN

Makubaliano haya yatagusa maeneo yafuatayo, kujengea uwezo wanachama wa MISA Tan kwenye kuandika habari jengefu, kuwa na programu za kubadilisha uzoefu baina ya wanachama wa MISA Tan na matawi ya nje ya Nchi ya PACJI, Kufanya tafiti Kwa pamoja na kushiriki kwenye mikutano ya kinataifa Kwa lengo la kusambaza falsafa ya uandishi wa habari jengefu

Kwa upande wa MISA Tan aliyesaini makubaliano hayo ni Mwenyekiti wa MISA Tan Bwana Edwin Soko na Kwa upande wa Taasisi ya PACJI aliyesaini ni Daktari David Mrisho, pia makubaliano hayo ni ya miaka mitatu yanayolenga kuzinufaisha Taasisi zote mbili ambayo yamefanyika kwenye hotel ya Royal Village Jijini Dodoma.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464