STEPHEN WASIRA APENYA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI CCM TAIFA
Saturday, January 18, 2025
Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, ameteuliwa kugombea nafasi ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa. Uteuzi huu unakuja baada ya Abdulrahman Kinana kujiuzulu nafasi hiyo.
Wasira, ambaye ni miongoni mwa viongozi wazoefu na wenye ushawishi mkubwa ndani ya chama, anapigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa unaoendelea Jijini Dodoma.
Uteuzi wake unalenga kuimarisha uongozi na kuendeleza mipango ya chama.