MADIWANI KISHAPU WAMEPITISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 BILIONI 41.6

MADIWANI KISHAPU WAMEPITISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 BILIONI 41.6

Na Marco Maduhu,KISHAPU

MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, wamepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, sh,bilioni 41.4,huku wakipongeza taarifa ya bajeti hiyo kuwa na uwazi na wameweza kuichangia vizuri.
Wamepitisha bajeti hiyo leo Januari 21,2025, kwenye Kikao cha Baraza cha Bajeti katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johson,akisoma taarifa hiyo ya makadirio ya mapato na matumizi katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, amesema wameomba kuidhinishiwa kukusanya kiasi cha fedha sh.bilioni 41.4 kutoka mapato ya ndani,serikali kuu na wadua wa maendeleo.
"Mheshimiwa Mwenyekiti katika mwaka wa fedha 2025/2026, halmashauri inaomba kuidhinishiwa kukusanya kiasi cha fedha sh.bilioni 41.4,"amesema Johson.

Amewapongeza pia Madiwani kwa kujadili taarifa hiyo vizuri na kutanguliza maslahi ya wananchi,na kwamba ushauri,maelekezo na mapendekezo yote ambayo wameyatoa atayafanyia kazi.
Nao Madiwani hao kwa pamoja walipitisha makadirio hayo ya bajeti,huku wakipongeza taarifa kuwa ya uwazi, kuliko bajeti zilizopita na wameweza kujadili kwa kina kwa maslahi mapana ya wananchi wa Kishapu.

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Andrew Kifua,akitoa salamu za viongozi kwenye baraza hilo, amewapongeza madiwani wa kujadili vyema na kuipitisha bajeti hiyo.
Amepongeza pia hoja za kuibua vyanzo vipya vya mapato,na kuwasihi Watendaji wa Halmashauri wakasimamie vizuri vyanzo hivyo ili Halmashauri ipate mapato.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Francis Manyanda,amewataka Watumishi wa Halmashauri hiyo kwamba wafanye kazi kwa bidii na juhudi zote ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato hayo.
Aidha,katika Baraza hilo la Madiwani walipitisha pia mpango wa mapendekezo ya bajeti ya matengenezo ya barabara (TARURA) katika mwaka huo wa fedha 2025/2026 kiasi cha sh.bilioni 2.3.

TAZAMA PICHA 👇👇
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonhson akizungumza kwenye Baraza hilo la Bajeti.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Francis Manyanda akizungumza kwenye Baraza hilo la Bajeti.
Mwakilisha wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Andrew Kifua akizungumza kwenye Baraza hilo la Bajeti.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Kishapu Jamali Namangaya akizungumza kwenye Baraza hilo la Bajeti.
Madiwani wilayani Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Bajeti.




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464