TIC YAITA WAWEKEZAJI KUWEKEZA SHINYANGA

TIC YAITA WAWEKEZAJI KUWEKEZA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KITUO cha uwekezaji Tanzania (TIC)kimewahamasisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, kuja kuwekezaji mkoani hapa,kutokana na kuwepo na mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na upatikanaji wa mahitaji yote,na utengwaji wa maeneo likiwamo la Buzwagi Economic Special zone wilayani Kahama.
Hayo yamebainishwa leo januari 23,2025 na Mwenyekiti wa Bodi ya TIC Dr. Binilith Mahenge,wakati wa ziara yao mkoani Shinyanga,pamoja na kutembelea Kiwanda cha uzalishaji mafuta ya kula cha Jielong Holding kilichopo Nhelegani Manispaa ya Shinyanga.

Amesema TIC wapo ziara mkoani Shinyanga, kwa kutembelea baadhi ya miradi ambavyo vimesajiliwa na Kituo hicho,ili kuona maendeleo yao, pamoja na kubaini changamoto ambazo zinawakabili,huku akielezea kuridhishwa na mazingira mazuri ya uwekezaji mkoani humo,na kuwaita wawekezaji wawekeze katika mkoa huo.
“Shinyanga ina mazingira mazuri ya uwekezaji,takwimu za mwaka 2023 ambazo TIC tulisajili miradi ilikuwa 500, lakini mwaka 2024 ilifika 901,na Mkoa huu unashika nafasi ya 10 kwa usajili wa miradi mwaka jana ilisajili miradi 16 kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara,”amesema Dr.Mahenge.

“Hii inaonyesha mkoa huo umeboresha mazingira mazuri ya uwekezaji,sababu kuna mahitaji yote muhimu ya kuvutia wawekezaji na wametenga maeneo,hivyo rai yangu kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi waje wawekeza hapa Shinyanga,”ameongeza.
Aidha,amewapongeza pia wawekezaji wa Kiwanda cha Jielong Holding kwa kuwekeza hapa nchini na kutoa ajira nyingi kwa vijana, kuinua uchumi wa wakulima pamoja na serikali kupata mapato,huku akiwasihi Wakulima wa Pamba kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao hilo, ili Kiwanda hicho kipate Malighafi ya kutosha na kuzalisha bidhaa nyingi.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,akitoa salamu za mkoa kwa wageni hao TIC,amesema Mkoa huo una mazingira mazuri ya kuwekeza, na una mahitaji yote ikiwamo miundombinu ya barabara,reli,uwanja wa ndege,umeme na maji ya kutosha.
“Tunakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza Shinyanga sababu mahitaji yote yapo,”amesema Macha.

Nao Wawekezaji wa Kiwanda cha Mafuta ya kula cha Jielong Holding ambao wametembelea na TIC,wameipongeza serikali kwa kuendelea kuwekeza mazingira mazuri ya uwekezaji, na kwamba wameendelea kupanua wigo wa kiwanda hicho kwa kuongeza mitambo mingine.

Msimamizi wa Kiwanda cha Jielong Qi Liaoyuan ambaye ni Raia wa chini,amesema Kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 2012 na kimetoa ajira nyingi, na kina uwezo wa kuzalishaTani 150,000 za mbegu za Pamba kwa ajili ya mafuta ya kula.
Amesema kwa sasa wamesimamisha uzalishaji wa mafuta hayo, mara baada ya kukosekana kwa Malighafi ya mbegu za pamba, na kwamba wanasubiri msimu uanze tena wa pamba ndipo waendelee na uzalishaji.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akitoa salamu za Mkoa huo katika ziara ya TIC.
Mwenyekiti wa Bodi ya TIC Dr. Binilith Mahenge akizungumza kwenye ziara hiyo.
Afisa Biashara Mkoa wa Shinyanga Rose Tungu akizungumza kwenye ziara hiyo ya TIC.
Mfanyakazi wa kiwanda cha Jielong Hassan Manubi akizungumzia faida ya uwekezaji.
Mkalimani wa Lugha ya Kichina Khadija Yusuph akisoma taarifa ya Kiwanda.
Msimamizi wa Kiwanda cha Jielong Qi Liaoyuan akizungumza katika ziara ya TIC.
Ziara ya TIC ikiendelea katika Kiwanda cha Jeilong cha uzalishaji Mafuta ya kula kwa kutumia Malighafi ya Mbegu za Pamba.
Ziara ya TIC ikiendelea katika Kiwanda cha Jeilong cha uzalishaji Mafuta ya kula kwa kutumia Malighafi ya Mbegu za Pamba.
Ziara ya TIC ikiendelea katika Kiwanda cha Jeilong cha uzalishaji Mafuta ya kula kwa kutumia Malighafi ya Mbegu za Pamba.
Ziara ya TIC  katika Kiwanda cha Jeilong cha uzalishaji Mafuta ya kula kwa kutumia Malighafi ya Mbegu za Pamba.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464