MABALA MLOLWA AZINDUA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA KUZALIWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KATIKA MKOA WA SHINYANGA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa,amezindua Rasmi sherehe za kuzaliwa kwa miaka 48 ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika mkoa huo,huku akitoa tamko la kuunga mkono Mkutano Mkuu wa CCM,kumpitisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea pekee wa Urais kwa tiketi ya Chama hicho kwenye uchaguzi Mkuu 2025.
Uzinduzi huo umefanyika leo januari 28,2025 katika Kata ya Kagongwa wilayani Kahama,ambao umeambatana na kuunga Mkono Azimio la Mkutano wa CCM Taifa la kumpitisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mabala akizungumza wakati wa kuzindua sherehe hizo,amesema kila kiongozi wa CCM kuanzia ngazi ya tawi watazifanya kwenye maeneo yao.
Amesema shughuli ambazo zitafanywa ni kuzungumza na wananchi,kuwaeleza mafanikio ambayo yamefanywa na Rais Samia,pamoja na kuwashukuru kwa kuwapigia kura wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,na kukipatia chama hicho ushindi wa kishindo.
"leo katika uwanja wa Kagongwa wilayani Kahama sherehe za kuzaliwa miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Shinyanga nazi zindua Rasmi na kelele chake kitakuwa Kishapu,"amesema Mabala.
Katika hatua nyingine Mabala,amesema kwaniaba ya wana CCM mkoa wa Shinyanga wanatoa tamko la kuunga mkono mkutano mkuu wa CCM taifa kwa ku azimia kumpitisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais pekee kupitia CCM kwenye uchaguzi mkuu 2025.
Ameongeza pamoja na Mgombea Mwenza Dk.Emmanuel Nchimbi na Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, kwamba wanafaa kwenye nafasi hizo katika kuwaongoza wananchi na kuwaletea maendeleo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya siasa Mkoa,amempongeza Rais Samia kwa kazi kubwa ambayo anaifanya mkoani humo katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Aidha,amewahidi wananchi wa Kagongwa kwamba serikali chini ya Rais Samia,itaendelea kuwaletea maendeleo pamoja na kutatua changamoto ambazo zinawakabili hasa za ubovu wa barabara.
Nao baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga akiwamo Idd Kassim wa Msalala,Emmanuel Cherehani wa Ushetu na Jummane Kishimba wa Msalala, wametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia, kwa kazi kubwa ambayo amefanya katika kuwaletea maendeleo wananchi kwenye majimbo yao na miradi mingi imetekelezwa.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha awali akisoma taarifa ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa niaba ya Katibu wa CCM Mkoa Odilia Batimayo,amesema Chama hicho kilianzishwa tarehe 5..2.1977 kutoka katika vyama viwili TANU na ASP,na kimefikisha miaka 48.
Uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM,pamoja na mambo mengine ziliambatana pia na ukataji wa keki ikiwa ni sehemu kumbukumbu ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alizaliwa tarehe 27.1.1960.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Muyonga akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mbunge wa Msalala Iddi Kassimu akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mbunge wa Kahama Mjini Jumanne Kishimba akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza kwenye uzinduzi wa sherehe hizo za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akitoa historia ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 1977.
Viongozi wakiwa meza kuu.