MAKOMBE AZINDUA RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 48 YA KUZALIWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KATIKA WILAYA YA SHINYANGA MJINI

MAKOMBE AZINDUA RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 48 YA KUZALIWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KATIKA WILAYA YA SHINYANGA MJINI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe,amezindua rasmi maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM)katika wilaya ya Shinyanga Mjini,huku wakiunga mkono maazimio ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, kwa kumpitisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,kuwa Mgombea pekee wa Urais kupitia tiketi ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu 2025.
Uzinduzi huo umefanyika leo januari 29,2025 katika Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama.

Makombe akizungumza kwenye uzinduzi huo,amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM),kimefanya mambo makubwa kwa wananchi,na sasa kinatimiza miaka 48, na kwamba wananchi wanapaswa kuendelea kukiamini na kukibakisha madarakani.
“Chama cha Mapinduzi CCM kimefanya mambo makubwa na kutekeleza miradi mbalimbali kwa wananchi ikiwamo ya kimkakati, na changamoto nyingi zimetatuliwa zikiwamo huduma za Afya,umeme ,maji, ujenzi wa shule na miundombinu ya barabara,”amesema Makombe.

“Katika awamu hii ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ametekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa asilimia 100, na zawadi pekee ambayo tunapaswa kumpatia wananchi wa Shinyanga, ni kumpigia kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu 2025 ili ashinde kwa kishindo,”ameongeza Makombe.
Katika hatua nyingine amesema, CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wanaunga mkono Azimio la Mkutano Mkuu Taifa, kwa kumpitisha Rais Dk.Samia Suluhu Haasan kuwa Mgombea pekee wa Urais kupitia tiketi ya CCM, kwenye uchaguzi Mkuu 2025 na Mgombea mwenza Dk.Emmanuel Nchimbi,pamoja na Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi.

Aidha,amewaomba wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na kumuunga mkono Rais Dk.Samia ili aendelee kuongoza nchi na kuwaletea maendeleo, na kwamba ndani ya miaka yake minne ya utawala amefanya mambo makubwa, hivyo anapaswa kuongezwa miaka mingine mitano,”Rais Samia...mitano tena.
Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani, amesisitiza suala la Rais Samia kuendelea kuungwa mkono, pamoja na wananchi kukiamini Chama cha Mapinduzi CCM,na kwamba Chama hicho ndiyo Chama imara cha kuwaletea maendeleo na kinatekeleza ilani yake kwa vitendo.

Ametolea mfano katika Manispaa ya Shinyanga, kwamba miradi mingi imetekelezwa chini ya Utawala wa CCM, ikiwamo ujenzi wa Masoko,Madarasa kila Kata,uboreshaji wa huduma za Afya,miundombinu ya barabara na madaraja.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha, ametoa historia ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM,kwamba kilianzishwa tarehe 5.2.1977 baada ya vyama viwili kuungana, Chama cha TANU na ASP ndipo ikazaliwa CCM kwa lengo la kuleta ukombozi.

Amesema katika Maadhimisho hayo ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM, zitakuwa zikifanyika shughuli mbalimbali za kijamii, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi,kuwashukuru kwa kuwapigia kura wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na Chama hicho kushinda kwa asilimia 99.
Amesema, pia viongozi watayasemea mazuri ambayo yamefanywa na Rais Samia juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,kusajili wanachama wapya, pamoja na kuendelea kujipanga katika uchaguzi mkuu 2025, ili waendelee kushika dola na kuwatumikia wananchi, sababu CCM ndiyo Chama pekee chenye kuwaletea maendeleo.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Shinyanga Mjini.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani akizungumza kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Shinyanga Mjini.
Diwani wa Mwawaza Juma Nkwambi akizungumza kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Shinyanga Mjini.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akizungumza kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Shinyanga Mjini.
Mwenyekiji wa CCM Kata ya Mwawaza Mabula Mayuya akizungumza kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Shinyanga Mjini.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Shinyanga Mjini.
Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini ukiendelea katika Kata ya Mwawaza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akipanda Mti katika shule ya Sekondari Mwawaza.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akipanda Mti.
Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini ukiendelea katika Kata ya Mwawaza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464