MISA Tan na TAKUKURU wateta
Mwandishi wetu
Dodoma
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini Mwa Afrika ( MISA Tan) Bwana Edwin Soko Leo amemtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Bwana Crispian Francis Chalamila na kufanya mazungumzo juu ya kufanya kazi Kwa pamoja likiwemo suala la kuendelea kuwashirikisha waandishi wa habari kwenye programu ya Marafiki wa TAKUKURU.
Hatua hiyo ni mwendelezo wa uongozi mpya wa bodi ya MISA Tanzania ya kuwatembelea wadau mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha na kupanua wigo wa kufanya kazi na wadau mbalimbali wakiwemo TAKUKURU
Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye ofisi za TAKUKURU Makao Makuu Dodoma
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464