RC MACHA AKABIDHI GARI 2 KWA KACU ZILIZOTOLEWA NA TADB ZENYE THAMANI YA MILIONI 380


RC MACHA AKABIDHI GARI 2 KWA KACU ZILIZOTOLEWA NA TADB ZENYE THAMANI YA MILIONI 380

KAHAMA DC

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekabidhi gari mbili (2) aina ya Tata zenye uwezo wa tani 25 kila moja na zenye thamani ya Tzs. Milioni 380 kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU LTD) kutoka kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa lengo la kuboresha shughuli za uzalishaji wa zao la pamba na utoaji huduma kwa wateja wao ambao ni wakulima na wananchi.

RC Macha amekabidhi gari hizo jana akiwa kwenye ziara ya usambazaji wa mbegu za pamba na viua dudu katika Wilaya ya Kahama mbapo pamoja na mambo mengine amewawasitiza viongozi wa KACU kuhakikisha zinatunzwa gari ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi kazi iliyokusudiwa ya kuboresha na kuinua zao la pamba sanjari na kuziwezesha kudumu muda mrefu.

“Pamoja na kuwapongeza sana TADB kwa kazi hii nzuri mliyoifanya, sasa niwasihi sana KACU mkazitunze hizi gari kwa kuwa zinaenda kuwasaidia ninyi zaidi KACU katika kuinua upya uzalishaji wa zao la pamba, kuboresha utoaji huduma, kuwafikia wateja wenu amabo ni wakulima na wananchi wa maeneo yenu,” amesema RC Macha.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya KACU Ndugu Emmanuel Nyambi ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa kuwapatia gari hizo kwani nitawasaidia kwenye uzalishaji na kuongeza thamani ya zao la Pamba kwa wanachama wao na kuongeza pato lao na Serikali kwa ujumla

Awali akitoa salamu za Benki, Afisa Mikopo kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Ndugu Andrew Ezekiel amesema kuwa hawana hofu kabisa na KACU katika utekelezaji wa majukumu yao huku akiwaasa kuwa na uangalizi na usimamizi mzuri na wa karibu zaidi ili kuhakikisha kiwanda cha KACU kinarudisha thamani na heshima ya zao la Pamba.

Katika hafla hiyo, RC Macha alikuwa ameambatana na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani @cherehaniemmanuel pamoja na wataalam mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464